HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 September 2018

ZOEZI LA UZIBAJI MIVUJO TABATA LAKAMILIKA KWA ASILIMIA 85- MHANDISI ARON

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamefunga zoezi la  siku tatu la uzibaji wa mivujo ya mabomba katika Mkoa wa Tabata na kufanikisha  kuziba mivujo 298 iliyokuwa sugu na mipya ikiwa ni mikakati ya siku 100 ya Dawasa mpya kuhakikisha wanaondoa tatizo hilo.


Zoezi hilo lililoanzia  Mkoa wa Dar es Salaam  katika maeneo ya Tabata zoezi limedumu kwa muda wa siku tatu na kufanikiwa kwa asilimia 85 kwenye kata zote 13.


Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa, zoezi hilo imeenda vizuri kwa mafundi wote kufanya kazi kwa ufanisi mzuri na kufanikisha kuziba mivujo yote 298 kwa asilimia 85 na tayari wameshakabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata.

Aron amesema,Tabata kulikuwa na changamoto kubwa sana ya Mivujo na wamefanikiwa kwa asilimia kubwa na kwa sasa wanahamia Ubungo kuanzia wiki ijayo na kuwataka mafundi waliofanikisha kuondoa changamoto ya mivujo Tabata kuwa ana imani watafanya kazi nzuri.


"Nina imani tunahamia Ubungo mafundi mtafanya kazi nzuri kama ya Tabata na hilo sina shaka, kwa takwimu Tabata kulikuwa kunaongoza kwa mivujo na hilo linatokana na kuwa na miundo mbinu chakavu ya muda nrefu na tumekabidhi kwa meneja wa Dawasa Tabata na tayari tumempa maelekezo kuwa mivujo yote itatakiwa kufanyika matengenezo ndani ya masaa 6,"amesema Aron.

Aliongezea na kusema, Dawasa mpya imeweka mikakati zaidi ya kuboresha miundo mbinu na  kuhakikisha ndani ya miaka mitatu miundo mbinu hiyo inabadilishwa ili wananchi wasikose maji na idara ya uzalishaji na usambazaji maji itahakikisha katika kipindi chote hicho watakuwa wanasimamia miundo mbinu hiyo ili kuondokana na uvujaji wa maji.

Akiongezea, Aron amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona maji yanavuja kupitia namba yao ambayo haina malipo pia hata watakapowaona mafundi wa Dawasa wawape taarifa ili wakarekebishe eneo hilo.

Meneja wa Dawasa Tabata Victoria Masele baada ya kukamilika katika kata zake zote 13 za Tabata amesema kuwa, anatambua eneo la Tabata lilikuwa limeathirika sana kwa mivujo kwani miundo mbinu yake ni ya zamani toka enzi ya Mchina na ilikaa muda mrefu bila maji  kwahiyo zoezi hili limesaidia kuondoka kero kwa asilimia 85.

Victoria amesema kuwa, tatizo la mivujo linatokana na mtandao wa maji kuwa mdogo na maji yanakuja kwa kasi kubwa sana yanapelekea kupasuka kwa mabomba ya maji  hasa katika maeneo ya Kimanga na Segerea.

"Mafundi wamefanya kazi kubwa sana wakifanikiwa kuziba mivujo 298  sawa na asilimia 85 na hiyo ambayo imebaki itaendelea kushughulikiwa kwani tayari mafundi wangu niimeshawaambia wahakikishe mivujo mipya na ile ya zamani irekebishwe ndani ya miezi 6,"amesema Victoria.

Amesema baada ya zoezi hili kukamilika anaamini uuzaji wa maji kwa wateja wake  utaongezeka  na kuchochea ongezeko la mapato kwenye Mamlaka pamoja na kuongeza wateja wapya  ambapo ndani ya siku 100 watarajia wateja 4000 kujiunga kwenye mtandao wao.

Meneja wa Usambazaji maji Mhandisi Paschael Fumbuka amesema zoezi hili ni kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ya maji kwa kuzuia upotevu wa maji kitu ambacho kinaathiri biashara ya maji maana kila tone la maji linahesabiwa na kwa sasa wanahamia Mkoa wa Ubungo mwishoni mwa wiki hii.

Fumbuka ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Dawasa kuwabaini watu wanaochafua miundo mbinu yao ikiwamo kutiririsha maji taka na hatua za kisheria zitachukuliwa juu yao.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph akizungumza na mafundi waliofanikisha kurekebisha kwa mivujo 298 katika Mkoa wa Tabata uliofanyika kwa siku tatu na kuwapongeza kwa kazi kubwa sana  walioifanya na kuwataka wajipange kwa Mkoa wa Ubungo.

Meneja wa Dawasa Tabata Victoria Masele (kulia) akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph na kuahidi kurekebisha mivujo yote ndani ya saa 6 kama alivyoagizwa baada ya kufanikisha kwa zoezi la uzibaji mivujo ndani ya Mkoa wake wa Tabata.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad