VYAMA vya siasa hapa Nchini vimetakiwa kudumisha na kuimarisha
demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi
imara tofauti na mawazo ya walio wengi kuwa vyama hivyo sio imara kiasi cha
kufananishwa na vikundi vidogo vidogo katika Jamii kama vile Saccos.
Hayo yalisemwa na Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji
Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa
vyama vya siasa kinachoendelea leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvijengea
vyama uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze
kujiendesha kama taasisi.
Jaji Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga
vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika
vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati chafu
kutoka Ofisi yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali.
‘’Mafunzo ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile
mali za vyama ni muhimu kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni
vyema mkatambua kuwa vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji
wa ndio maana msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji
Mtungi.
Aidha Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa
kuwa elimu ya fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili
linasaidia sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.
Wakati huo huo Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es
Salaam Profesa Rwekaza Mkandala ambaye aliwasilisha mada ya Jinsi ya Kuendesha
chama kama taasisi,amesema lengo la chama cha siasa chochote ni kujiandaa
kushika madaraka au kuwa wapinzani wa serikali hivyo lazima kuhakikisha
vinajijenga kama taasisi inayoaminika kwa wananchi.
Profesa Mkandala amesema siasa vyama vingi hapa Nchini ni
matokeo ya ukoloni mamboleo ambao ulianza kushamiri hapa nchini kwa miaka 1990
ambapo nchi ya Tanzania kama zilivyo nchi nyingine Barani Afrika zilikumbwa na
mabadiliko ya kiuchumi ya soko huria ikiwemo nchi zilizokuwa za ujamaa kuanza
kufuata m asharti ya Shirika la Fedha Duniani IMF.
Aidha
Profesa Mkandala alitaja vigezo vinavyofanya chama kuwa Taasisi muhimu kuwa ni
Itikadi, Uongozi bora, Wanachama, Sera na programu za chama, Rasilimali
Msajili wa vyama vya siasa,Jaji Francis Mutungi akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Msajili msaidizi Sisty Nyahoza akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa katika semina ya siku mbili leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam
Profesa Rwekaza Mkandala akizungumza na viongizi wa vyama vya siasa kuhusu jinsi ya kujiendesha chama kama taasisi.
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika sema iliyofanyika lao.
No comments:
Post a Comment