HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 22 September 2018

UP DATES AJALI YA KIVUKO MV. NYERERE: Idadi ya miili iyoopolewa majini imefikia 163 ,miili 116 imetambuliwa na ndugu zao

 Sehemu ya waokoaji wakiwa katika pemezoni mwa kivuko cha Mv. Nyerere kilichopinduka na kupelekea idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na wengine kujerukiwa, katika eneo la Ukara, Kisiwa cha Ukerewe jijini Mwanza, wakiangalia maeneo mbalimbali kutafuta miili au watu waliohai waliozama kwenye maji. ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka juzi Alhamisi (Septemba 20, 2018) kikikadiriwa kubeba idadi kubwa ya abiria kuzidi uwezo wake. Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mpaka wahati huu miili ya waliopolewa majini imefikia 163, huku kati yao miili 116 imetambuliwa na ndugu zao. Picha zote na Steve Magombeka a.k.a Kasampaida.
 Vivuko vya Mv. Clarias na Mv. Nyehunge vikiwa tayari kwa msaada wowote wa hata.
 Baadhi ya vijana wa Skaut wakiwa wamebeba moja ya miili iliyoopolewa kwenye maji baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka.
Zoezi la Ukoaji likiendelea.


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad