HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 5 September 2018

UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA

Jopo la majaji wa Tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2018 limemtangaza Mwandishi wa habari I wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2018.
Tuzo hiyo imetangazwa leo Jumanne Septemba 4,2018 wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.
Kushoto ni Absalom Kibanda Mhariri mkuu kutoka gazeti la. Mtanzania akikabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi 2018 kwa mke wa Azory Gwanda.Katikati ni rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mke wa Azory Gwanda
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage akitangaza mshindi wa tuzo ya Mwangosi 2018.
Mbali na kukabidhiwa tuzo hiyo,pia amekabidhiwa cheti cha utambuzi pamoja na shilingi milioni 10.
Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, wakwanza kulia ni mwenyekiti wa jopo hiloNdimara Tegambwage, Katikati ni mama Edda Sanga, na wengine wawili. 

Na Seif Mangwangi,Arusha
UMOJA wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), imemtangaza Mwandishi Azory Gwanda ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba mwaka jana kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi kwa mwaka 2018.

Gwanda aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya mwananchi communication akiandikia gazeti la Mwananchi alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika kazi zake za kihabari katika maeneo ya Kibiti na Rufiji.

Tuzo hiyo ya Daudi Mwangosi sambamba na kiasi cha shilingi milioni kumi (10), alikabidhiwa mke wa Gwanda, katika mkutano mkuu wa mwaka wa UTPC.

Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo, Absolom Kibanda aliiomba Serikali kutofumbia macho matukio ya utekaji wa waandishi wa habari kwa kuwa yanatoa ishara mbaya kwa jamii na kuminya uhuru wa habari.

Alisema Rais Dkt John Magufuli amekuwa rafiki mkubwa wa vyombo vya habari hivyo alimtaka kutoishia kuwa rafiki na badala yake achukue hatua dhidi ya matukio ya utekwaji na kuteswa kwa waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad