HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 14 September 2018

UBALOZI WA CHINA WAMKABIDHI ZAWADI DK.TULIA


Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kwa ajili ya washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipokea hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kutoka kwa Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akisainiana hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozini hapo jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jini Mbeya. 
(Picha na Muhidin Sufiani)

*Ni kwa ajili ya washindi wa Tulia Traditional Dances Festival 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust Dk.Tulia Akson ameushukuru Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kumkabidhi pikipiki 10 kwa ajili ya washindi watakaopatikana kwenye tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018.

Dk.Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge amekabidhiwa pikipiki hizo leo katika ubalozi huo na Mwakilishi wa Balozi wa China Tanzania nchini Xu Chen.Thamani ya pikipiki hizo ni Sh.milioni 21,600,000.

Akizungumza baada ya kupokea pikipiki hizo Dk.Tulia amesema anaushukuru ubalozi huo kwa kutoa zawadi hizo kwa ajili ya washindi wa tamasha hilo litakalofanyika kuanzia Septemba 18 hadi Septemba 22 mkoani Mbeya.

“Kwa niaba ya Taasisi ya Tulia Trust tunatoa shukrani zetu kwa ubalozi wa China nchini Tanzania kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi kwa kutoa zawadi kwa ajili ya washindi.

“Mwaka jana walitoa pikipiki 10 ambazo tulikabidhi kwa washindi.Lengo la tamasha hili ni kukuza utamaduni wetu na tumeanza na ngoma za asili.Pia  tunataka wanaoshiriki pia wajikwamue kiuchumi,”amesema Dk.Akson.

Akifafanua zaidi kuhusu zawadi kwa washindi Dk.Askon amesema mshindi wa kwanza kwa idadi iliyopo watapata zawadi na kwamba jumla ya vikundi 108 vitashiriki.

Pia amesema tamasha hilo ni endelevu na linafanyika kwa mara ya tatu mfululizo na lengo kuu ni kukuza utamaduni wetu, pia iwe sehemu ya kuwawezesha wananchi kujenga uchumi,”amesema.

Amefafanua kama mwaka jana kuna kikundi kilishinda na kupata zawadi maana yake watakuwa wamepiga hatua kiuchumi na iwapo mwaka huu watashinda tena pia watapata pikipiki ya pili.

“Naomba nishukuru tena kwa namna China ambavyo wanathamini na kutambua utamaduni wetu na hivyo kuwa sehemu ya kuhakikisha tunafanikisha,”amesema Dk.Tulia Akson.
Ametoa ombi kwa ubalozi wa China iwapo wataona inafaa kuongeza idadi ya pikipiki kwa tamasha la mwakani kwani idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Kwa upande wake Naibu Balozi wa China nchini Tanzania Xu Chen amesema wanatambua nchi hizo mbili kila mmoja imekuwa na umataduni wake na ipo haja ya kuona kila nchi inaendeleza utamaduni huo.

Amefafanua utamaduni ni utambulisho wa Taifa lolote na hivyo ni vema ukapewa nafasi ya kuendelezwa na kwa kutambua hilo wameona umuhimu wa kuwa sehemu ya kufanikisha tamasha hilo.

Pia  Chen ampongeza Dk.Tulia Akson kwa namna ambavyo amekuwa akionesha umahiri wake katika masuala ya utamaduni kwani wamemshuhudia mara kadhaa akicheza jukwaani na hasa kwenye shughuli ambazo zinahusiana na Bunge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad