HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 3, 2018

TAWLA yaanzisha kampeni ya kuandika wosia kwa wamasai na wameru

 Wananchi wa kata ya Olmotonyi wakiwasikiliz Mafisa sheria wa chama cha wanawasheria wanawake (Tawla), Neema Ahmed, na Aika Palangyo katika kampeni kuhusu suala la uandishi wa wosia.
 Wananchi wa kata ya Olmotonyi wakimsikiliz afisa sheria wa chama cha wanawasheria wanawake (Tawla), Neema Ahmed ( hayupo pichani), akiwahamasisha kuhusu suala la uandishi wa wosia.
Mwanasheria wa Tawla Aika Palangyo aliwaeleza wakazi wa kata ya Olmotonyi namna wosia unavyoandikwa.

Seif Mangwangi, Arusha
CHAMA cha wanasheria wanawake (Tawla), kimeanza kampeni ya kuhamasisha Jamii ya kabila la  maasai na wameru kuandika wosia kabla ya kufariki dunia kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya unyanyasaji baada ya mmoja katika familia kufariki.

Akizungumza jana katika kampeni hiyo iliyofanyika kwa wananchi wa vijiji vya ngaramtoni, emaoi na olmotonyi katika kata ya olmotonyi wilayani Arumeru, Afisa sheria kutoka Tawla, Neema Ahmed alisema ofisi yao imekuwa ikipokea matukio mengi ya wanawake kunyanyaswa baada ya waume zao kufariki.

Alisema wajane katika familia nyingi za jamii ya kimaasai na kimeru wamekuwa mafukara kutokana na kunyang’anywa mali na mashemeji mara baada ya waume zao kufariki dunia bila kuacha maandishi yanaayoonyesha urithi wa mali.

“Lakini cha kushangaza hizi mali zinazogombewa unakuta ulizitafuta na mme wako lakini inapotokea ukafariki dunia wanaibuka mashemeji na hata wakati mwingine wakwe wanawanyang’anya, sasa kama kutakuwa na wosia hakuna atakaeweza kuingilia mali za marehemu, “ alisema.

Neema alisema mila nyingi za jamii hizo zimekuwa zikikandamiza haki za wanawake lakini suluhisho la mila hizo ni wosia ambao hueleza warithi halali wa mali za marehemu baada ya kufariki na kuepusha migogoro.

Hata hivyo aliwaeleza wakazi hao kuwa ni muhimu kuwashirikisha wanasheria wakati wa kuandika wosia kwa kuwa wosia ni siri ya mtu  ili kuwa shahidi wakati kifo kinapotokea na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Olmotonyi, Judica Elisha Lukumay alisema mafunzo kuhusiana na uandishi wa wosia ni muhimu sana kwa jamii hiyo kwa kuwaa wanawake wamekuwa wakinyanyasika sana.
Alisema jamii ya kimaasai na wameru wamekuwa na uelewa mdogo kuhusiana na uandishi wa wosia jambo ambalo limekuwa likisababisha wanawake na watoto kunyanyasika baada ya Baba kufariki katika familia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad