HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 24, 2018

SHULE YA QUEEN’S KUJENGA MAABARA YA SAYANSI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NA AWALI

Meneja wa Shule ya Msingi na Awali ya Queen’s Anna Mwalongo akizungumza kuhusiana na shule hiyo kufanya vizuri katika matokeo kwa wanafunzi wanaosoma hapo.  
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza katika mahafali ya Nane katika Shule ya Msingi na Awali ya Queen’s iliyopo Ukonga Tabata jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Shule ya Queen’s Lilian Wassira akizungumza kuhusiana na uwekezaji wa shule hiyo ikiwa ni pamoja kusomesha watoto 30 kutoka moja ya vituo vya watoto yatima na wanaoishi na kufanya kazi mtaani. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikata Keki kwa ajili ya wahitimu na wazazi katika shule ya Queen’s.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Queen’s Samweli Mwakipesile akizungumza kuhusiana na ujenzi wa Ghorofa kwa ajili ya mabara ya komputa katika shule hiyo.
 Wanafunzi wa Shule ya Queen’s wakitupwiza katika mahafali ya Nane ya Shule hiyo. 
 Wanafunzi wa Shule ya Queen’s wakiendesha mfano wa bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni kionjo katika mahafali ya Nane ya shule hiyo.
Mkurugenzi wa Shule ya Queen’s Lilian Wassira akiwa amenyanyua mkono kwa ajili ya kuwashukuru walimu wa shule hiyo katika picha hiyo ya pamoja.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema kuanzishwa kwa maabara ya sayansi kwa ngazi ya shule za msingi kutasaidia upatikanaji wa wataalamu wa fani hiyo nchini badala ya wataalamu hao kutokana nje ya nchi. 

Mjema amesema hayo jijini Dar es salaam Septemba 22 wakati wa akiweka  jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kompyuta, ukumbi na mkataba ya shule katika shule ya msingi na awali Queen's pamoja na mahafali ya nane kwa wanafunzi wa awali na darasa la saba. 

Amesema si Mara nyingi sana shule za awali na msingi wakawa na maabara watoto wanaanza wakiwa wachanga watakapofika sekondari watakua wazuri sana ukizingati tuko katika serikali ya uchumi wa viwanda. 

" Tunaanza kuwajenga watoto sasa hivi sisi tunataka kama serikali wataalamu hawa watakua Wahandisi na marubani ambao watatumika maeneo mbalimbali ya viwanda watatoka hapa hapa nchini na hatutaweza kuwategemea wataalamu kutokana nje ya nchi waje hapa" amesema Mjema. 

Aidha ameongeza kuwa wao kama serikali wameunga mkono jitihada hiyo, hivyo shule nyingi zitaanza kuiga mfano wa shule ya msingi ya Queen's ya kuwa na maabara kwa ngazi ya awali na serikali wanampango wa kuanzisha programu hiyo. 

" Serikali tuna mipango mingi tukipata wadau kama nyinyi ambao mtatusaidia hilo litakua jambo pekee sana kwetu" ameongeza Bi Mjema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule ya Msingi na awali Queen's Bi Lilian wasira amesema wako hawako kibiashara, shule ipo kwa akili ya kuendeleza elimu kwa jamii wanataka kutengeneza kizazi cha taifa la kesho 

Nae meneja wa shule hiyo Bi Anna Mwalongo amesema wamejipanga kutoa taaluma ambayo inakidhi viwango vya elimu nchini na pia shule inawalea watoto yatima na wanaishi katika mazingira magumu wapata 30. 

"Ni muhimu sana kutokana na teknilojia tuliyonayo ya ulimwengu huu, ya sayansi wakajifunza mapema na watoto wengine wana vipaji vyao, pia maabara hii itawasaidia wanafunzi wa nje ya shule waliohitimu shule" amesema Bi Mwalongo. 

Amesema shule ilipata hasara kwa miaka kadhaa iliyopita ikashindwa kujiendesha kwa faida, hivyo kwa sasa wamejipanga vyema katika kuhakikisha wanatoa huduma bora ya elimu kwa jamii. 


Hii ni mahafali ya nane ya Shule ya msingi na awali Quen's ambapo shule hiyo ilianzishwa mwaka 1998 na kupata usajili wake wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2004. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad