HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 12 September 2018

NCHI ZA AFRIKA ZAENDELEA KUWA NA UHABA WA MBEGU ZA MSINGI

 Meneja Biashara Wycliffe Ingoi kutoka kampuni QualiBasic seed Company Ltd yenye makao yake nchini Kenya Na. Vero Ignatus, Arusha.
Kutoka kushoto ni Msemaji wa Mradi kutoka kampuni ya African Agriculture Technology Foundation (AATF) ya nchini Kenya Kenya Everlyn Situma, akiwa na Meneja Biashara Wycliffe Ingoi kutoka kampuni QualiBasic seed Company Ltd yenye makao yake nchini Kenya wakizungumza na waandishi wa habari leo. Picha na Vero Ignatus

Na. Vero Ignatus, Arusha.
Imeelezwa kuwa uhaba wa mbegu za misingi utaendelea kuwa tatizo katika nchi za Afrika kutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu hizo

Hayo yameelezwa leo na meneja biashara Wycliffe Ingoi kutoka kampuni QualiBasic seed Company Ltd yenye makao yake nchini Kenya wakati akitoa taarifa hiyo ya hali halisi ya upatikanaji wa mbegu hizo kwa vyombo vya bahari Jijini Arusha.

Ameongeza kuwa kutokana na uzalishaji wa mbegu hizo za msingi ambapo kampuni nyingi za uzalishaji wa mbegu kutokumudu gharama za uongezaji ubora katika mbegu hizo

Aidha amesema kuwa hivi sasa kuna kampuni moja tu inayoongeza ubora wa mbegu hali ambayo hailingani na mahitaji ya mbegu za msingi kwa wakulima.

Kwa upande wake Msemaji wa Mradi kutoka kampuni ya African Agriculture Technology Foundation (AATF) ya nchini Kenya Everlyn Situma ameiomba serikali nchini Tanzania kupitia watafiti wa mbegu kuweza kuangalia namna ambayo wanaweza kuruhusu mbegu za mahindi zanye kinga kutumiwa kwa wakulima

Ameitaka jamii kubadili mtazamo hasi ambao wengi wao wamekuwa wakidhania mbegu hizo zenye kinga zina mbalimbali ikiwemo kansa na utasa kwa wanaume na wanawake.

Amesema utafiti umefanyika kwa nchi 12 barani Afrika ambao unaonyesha mbegu hizo ni salama kwa matumizi ya kilimo na kuzuia mazao kushambulia na wadudu.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad