Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSIMU wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zimezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es salaam na kumtangaza kwa Mlezi wa tuzo hizo.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alitangazwa kuwa mlezi wa tuzo za SZIFF kwa msimu wa pili na kuahidi kuhamasisha vijana kujikita zaidi katika ubunifu wa sanaa ya uigizaji.
Akizindua maandalizi ya tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa anajivunia namna msimu wa kwanza wa tamasha la SZIFF lilivyoamsha ari na hamasa kwa waandaaji na wapenzi wa filamu nchini na fainali yake kufanyika 23 februari 2019.
Tido amesema, Hili ni tamasha la kwanza la Filamu Afrika kuonyeshwa kwenye televisheni , filamu zitashindanishwa kwenye vipengele tofauti huku ushindani ukiaminika kuwa mkubwa zaidi wa msimu uliopita kwakuwa moja ya vigezo vya filamu zitakazoshindanishwa ni kuwa lazima ziwe zimeandaliwa kati ya mwaka 2016 hadi 2018.
Amesema kuwa, mbali na hilo kwa mwaka huu wameongeza vipenele vingine vitano na kufikisha idadi ya tuzo zinazowaniwa kuwa 24, pamoja na mshindi kuondoka na tuzo hiyo pia atakabidhiwa kiasi cha fedha taslimu kulngana na nafasi alizowania na kushinda.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na Mlezi wa Tuzo za SZIFF Jokate Mwegelo amesema kuwa anafurahi sana kupewa nafasi ya kuwa mlezi wa tuzo hizo kwani hata yeye alikuwa katika tasnia ya filamu akiwa amecheza filamu mbalimbali.
Amesema kuwa, tuzo hizi zimeleta chachu ya wasanii kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa na kuhamasisha zaidi vijana kufanya kazi za sanaa kwani inawapatia kipato wasanii wengi sana ila wanahitaji mtu wa kuwasaidia kuinua na tuzo hizi za SZIFF zimekuwa na mchango mkubwa sana.
Mkurugenzi wa Tamasha la SZIFF, Jacob Joseph amesema kuwa kiswahili ni miongoni mwa ligha kumi kubwa kuzungumzwa Barani Afrikla, matamasha mengi hayajakidhi kuwafikia watu wengi na kuwatimizia mahitaji yao kupitia sanaa.
Aidha, Jacob ameongezea kuwa tamthilia kwenye televisheni zimejizolea umaarufu mkubwa kuwa watazamaji, hivyo uli kupima ufanisi wake mwaka huu kimeongezeka kipengele kipya cha tamthilia kwenye tamasha kijulikanacho kama Tuzo za tamthilia za kimataifa za Azam TV, tuzo hizi zitatolewa kwa tamthilia Bora, muongozaji bora, muandishi bora, muigizaji bora wa kike na wa kiume.
Kwa upande wa mratibu wa tamasha la SZIFF, Sophia Mgaza amesema kuwa dhumuni kuu ni kuleta soko la filamu na televisheni pamoja chini ya mwamvuli mmoja, Lugha moja , tamasha moja.
Amesema kuwa, waandaaji wanatakiwa kuwasilisha kazi zao za kiubunifu kwa ajili ya tamasha hilo na uwasilishwaji utaanza rasmi Oktoba Mosi 2018 mpaka 30 Novemba 2018 na vigezo vitakavyokuwa vinatumika ni kazi hiyo kuwa imesajiliwa COSOTA na Bodi ya Filami Tanzania.
Katika tuzo hizo, Mwenyekiti wa jopo la majaji ni Profesa Martin Mhando na mchakato huo wa tuzo utasimamiwa na jopo la majaji ambao watachambua kuainisha washindi kulingana na vigezo vilivyoweka.
fisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) na kumtangaza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kuwa mlezi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na wasanii waliojitokeza katika uzinduzi wa msimu wa pili pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) na kwuashukuru waandaaji wa tamasha hilo lwa kumpa nafasi ya kwua mlezi wao.
Mratibu wa tamasha la Sinema Zetu Nchini (SZIFF), Sophia Mgaza
akivitaja vigezo na tuzo zitakazowaniawa katika msimu wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu.
No comments:
Post a Comment