HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 20 September 2018

Mradi mpya wa utafiti kujenga uwezo kukabili mabadiliko tabia nchi wazinduliwa

 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida mara baada ya kuwasili katika ofisi za ESRF kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akiwa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto), Msimamizi wa mradi wa AFRICAP kwa Tanzania na Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi –ESRF, Bi. Vivian Kazi (kushoto), Mwakilishi wa, FANRPAN – AFRICAP anayeshughulikia sera (kikanda), Bi. Sithembile Ndema Mwamakamba (wa pili kulia) pamoja na Dr. Susanna Sally kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza wakiwa meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (hayupo pichani) na washiriki wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akitoa hotuba kabla ya kuzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimpongeza mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba kwa hotuba nzuri wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (katikati) akizundua rasmi mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto), Msimamizi wa mradi wa AFRICAP kwa Tanzania na Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi –ESRF, Bi. Vivian Kazi (kushoto), Mwakilishi wa, FANRPAN – AFRICAP anayeshughulikia sera (kikanda), Bi. Sithembile Ndema Mwamakamba (wa pili kulia) pamoja na Dr. Susanna Sally (kulia) kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza wakishuhudia tukio hilo.

 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akisoma yaliyomo kwenye kijarida cha mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania mara baada ya kuzindua mradi huo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam. Aliyeshika kipaza sauti ni Mwezeshaji wa hafla ya uzinduzi huo, Bw. Abdallah Henku (kushoto).
Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (katikati) akigawa vijarida vya mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania kwa washiriki mara baada ya kuzindua katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam
 Mwakilishi wa, FANRPAN – AFRICAP anayeshughulikia sera (kikanda), Bi. Sithembile Ndema Mwamakamba akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Muhamo Chisvo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Dr. Susanna Sally kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa kilimo cha kisasa kincahozingatia mabadiliko ya hali ya hewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi ya taarifa za hali ya hewa TMA kutoka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa maoni wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Dr. Steward Jennings kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza akiwasilisha mada kuhusu utengenezaji wa mifumo  na njia za kufanya kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya hali ya hewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Bw. Rob Bailey kutoka Chatham House nchini Uingereza akiwasilisha mada kuhusu utengenezaji na utekelezaji wa sera wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya kilimo kutoka, vyuo vikuu, taasisi mbalimbali za serikali pamoja sekta binafsi walioshiriki hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
MRADI mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania umezinduliwa jana.
Akizindua mradi huo ofisi za Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii –ESRF, Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba  alisema mradi huo unakuja wakati muhimu ambapo taifa linajikita katika kuelekea uchumi wa kati unaotegemea kilimo.
“Sekta ya kilimo imeendelea kuwa ni Sekta muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla hususan katika wakati huu Tanzania inapojizatiti kuelekea uchumi wa viwanda,” alisema Waziri Tizeba huku akisema kwamba sekta ya Kilimo iimekuwa ikiendelea kukua kwa kuchangia asilimia 30 ya fedha za kigeni na kuchangia malighafi za viwanda kwa asilimia 65.
Mradi huo umezinduliwa takaribani miezi mitatu baada ya wizara kuzindua rasmi Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II), yenye lengo la kuleta mageuzi ya Sekta ya kilimo (kilimo, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo.
Pamoja na kufanya uzinduzi huo aliipongeza ESRF na timu nzima ya mradi wa GCRF-AFRICAP kwa kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo kupitia tafiti na kujenga uwezo kwa lengo la kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kwa makundi ya jamii yaliyokua kwenye hatari zaidi.
Alisema Wizara yake itaendelea kukuza na kulinda maendeleo ya sekta ya kilimo yaliyo endelevu, kwa kuongeza uzalishaji, kuboresha mifumo ya kilimo inayokwenda sambamba na mabadiliko ya tabia nchi.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazingatia tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa umakini mkubwa sana, na Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambazo zimefanikiwa kuendeleza Mpango Mkakati wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi,  ili kwenda sambamba na dira ya maendeleo ya taifa 2025.” Alisema Dk. Tizeba.
Awali akimkaribisha Waziri Tizeba, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida alisema uzinduzi wa mradi wa utafiti na wa kujenga uwezo katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania, ujilikanao kama GCRF-AFRICAP, ni hatua muhimu  kwa mustakabali wa sekta ya kilimo nchini.
Alisema mradi wa GCRF-AFRICAP ni mradi wa kikanda utakaojumuisha nchi nne Barani Afrika, ambazo ni Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Zambia huku ESRF ikiwa ndiye msimamizi kwa upande wa Tanzania.
Dk. Kida alisema lengo kuu la mradi ni kuainisha na kutekeleza sera zinazotokana na uthibitisho wa kisayansi kupitia utafiti katika kuendeleza maendeleo endelevu, uzalishaji, mifumo ya Kilimo inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha kufikia usalama wa chakula na maendeleo ya Kiuchumi.
“Kiini cha mradi huu ni kuainisha mustakabali wa mifumo ya kilimo na chakula nchini ili kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima walio katika hatari zaidi ya kuathiriwa na mabadiliko hayo katika sekta ya kilimo.” Alisema Dk Kida.
Aidha alisema kwa kuzingatia tishio la mabadiliko ya tabia nchi, mradi pia utajenga mahusiano endelevu baina ya Mamlaka ya hali ya hewa nchini, Taasisi za Utafiti za Kilimo, na vyuo vikuu katika nchi za Tanzania, Zambia, Malawi, na Afrika Kusini .
Naye Mwakilishi wa, FANRPAN – AFRICAP anayeshughulikia sera (kikanda) Sithembile Ndema Mwamakamba akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Muhamo Chisvo alisema uzinduzi wa mradi huo ni hatua kubwa katika kutoa uwezo  wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kwamba maamuzi ya kuleta mradi huo Tanzania miongoni mwa nchi nne kumefanywa kwa sababu ya kuwapo kwa dhamira ndani ya serikali ya kutekeleza makubaliano ya kitaifa kuhusu kukabili mabadiliko ya tabianchi.
Alisema taasisi yake ni jukwaa ambapo wadau wanalitumia kujadiliana mambo muhimu na ya msingi yanayotishia mazingira.
Alisema lengo la FANRPAN ni kuwa jukwaa katika namna ambayo si rasmi kujadili mambo ya msingi yanatoishia maisha ya watu.
Amesema  lengo kuu ni kuendesha kilimo cha kisasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni sehemu ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad