HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 25 September 2018

MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO

 Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja (kulia) akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(katikati) mara baada ya kuwawasili katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuzungumza na viongozi mbalimbali. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkaribisha Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja ili aweze kuzungumza na viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora. 
 Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja akizungumza na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya(kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora. 
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora wakisikiliza Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja (hayupo katika picha) wakati alipotembelea Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya( wa tatu kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( wa tatu kutoka kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa mara baada ya kutembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja(kulia) akipiga saluti wakati akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo na viongoiz mbalimbali wa  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya akuzungumza na viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati wa Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Na Tiganya Vincent
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa Serikali Mkoani Tabora kwa kufanya kazi zao kwa ushirikiano ambao umesaidia kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao.

Alisema vyombo hivyo vinapaswa kuwa kitu kimoja jambo ambalo litawasaidia kubadilishana taarifa ili kufichua vikundi vya kihalifu kwa ajili ya kuhakikisha amani na salama miongoni mwa wananchi.

Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Masanja alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Viongozi wa Serikali , Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alipotembelea Ofisi ya Mkoa wa Tabora.

“Sio kila chombo kiende njia yake lazima kuwepo na umoja na mshikamano katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi” alisema.

Aliongeza kuwa na kila  Wananchi analo jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi kwa kuchukua hatua za kutoa taarifa juu ya  vikundi vya uhalifu katika maeneo yao ambazo zitaviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kuzuia uhalifu.

Meja Jenerali Masanja alisema kila mtanzania ni mdau wa kuhakikisha amani na usalama wa nchi kwa kuchukua hatua anapoona vitendo visivyofaa katika jamii na vinavyohatarisha amani.

Katika hatua nyingine Meja Jenerali Masanja alivitaka vyombo hivyo kuhakikisha vinajitahidi kusuluhisho migogoro na matatizo yanayojitokeza kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya alisema Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na ushirikiano mzuri na viongozi wa kuanzia Mkoa hadi Wilaya jambo ambalo limesaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad