HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 27 September 2018

MAWAKALA WA FORODHA WAELIMISHWA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI

Na Avila Kakingo, Globu ya jamii.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewaelimisha Mawakala wa Forodha  mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018.

Akizungumza wakati wa semina ya mawakala hao, Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala Tanzania (TAFFA), Tony Swai  amesema kuwa ujio wa sheria hii utapunguza na kuongeza Ushuru wa Forodha kwa baadhi ya bidhaa zinazoingizwa hapa nchini. 

"Maboresho ya sheria hiyo itasaidia nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukusanya kodi kwa urahisi na hatimaye kuongeza ukusanyaji mapato kwa kila nchi husika," alisema Swai.

Aidha, Swai amewaomba mawakala hao kutoa taarifa sahihi kuhusu bidhaa zinazoingia nchini na kulipa ushuru wa forodha na kodi stahiki kwa maendeleo ya Taifa. 

Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Juma Hassan amesema kuwa, uboreshaji wa Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki utasaidia uingizwaji wa malighafi ambazo zitasaidia utengenezaji wa bidhaa za ndani kwa gharama nafuu ili kukuza Uchumi wa Viwanda hapa  nchini na kupelekea bidhaa za ndani kuwa na gharama nafuu. 

Amesema wakala wa forodha watasaidia zaidi utekelezaji wa Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki kwa kushiriki na kusimamia bidhaa zinazoingizwa hapa nchini.

Kwa wakati tofauti, baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kuwa, mawazo waliyoyatoa yakifanyiwa kazi na TRA yatasaidia kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya serikali. 
 Kaimu Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Juma Hassan akizungumza na wananchama wa chama cha mawakala wa Forodha jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwajengea uwezo wanachama hao kuhusu sheria ya forodha na mapato ya Afrika Mashariki.
 Meneja msaidizikituo cha huduma cha Forodha Oswald Masawe akizungumza na waandishi wa haabari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwajengea uelewa wanachama cha mawakala wa forodha kuijua sheria ya mapato ya Afrika Mashariki.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala Tanzania (TAFFA), Tony Swai  akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa chama cha Forodha jijini Dar es Salaam leo.

 Baadhi  ya wanachama wa Chama cha Mawakala Tanzania wakichangia maada juu ya sheria ya Afrika Mashariki ya forodha. Baadhi  ya wanachama wa Chama cha Mawakala Tanzania wakisikiliza maada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad