HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 3 September 2018

MANONGA QUEENS YAILAZA SINGIDA WORRIER MECHI YA KIRAFIKI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TIMU ya Wanawake ya Mkoani Tabora katika jimbo la Manonga maarufu kama Manonga Queens wameichapa timu ya Singida Worrier bao 2-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja Namfua Mkoani Singida.

Manonga Queens walianza kuchungulia nyavu za Singida Worrier mnamo dakika ya 32 na waliandika bao la kwanza kupitia Ashura Shaabani.

Katika kipindi cha pili Singida Worrier walipata pigo la pili baada ya Ashura Shaban kwa mara nyingine kuifungia timu yake bao la pili mnamo dakika ya 85, na matokeo hayo yalidumu hadi dakika 90 zilipokamilika na Manonga Queens kutoa kifua mbele dhidi ya wwnyeji wao Singida Worrier.

Akizungumza baada ya mtanange huo kocha wa Manonga Queens Khamis Abihud amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa mgumu wachezaji walijituma na kuibuka na ushindi huo mnono ukiwa ugenini na ameeleza kuwa wamejizatiti katika kufuzu ligi kuu daraja la kwanza.

Ashura Shaban ambaye aliipatia timu yake mabao 2 ameeleza kuwa mazoezi, maagizo ya mwalimu na ushirikiano kutoka kwa wadau hasa Mbunge wa Manonga Seif Gulamali unazidi kuwapa ari na kasi zaidi ya kujituma katika soka.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali(katikati) akikabidhi mipira kwa viongozi na wachezaji wa Manonga Queens timu ya jimboni hapo ambayo inashiriki mpira ligi daraja la kwanza kwa wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad