Na Frank Mvungi- MAELEZO
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa
Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali
ya Awamu ya Tano kila wanapofanya maamuzi.
Akizungumza
leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa
Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa wanalo jukumu kubwa la
kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi
wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
“Nafasi
zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati
mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.”
Alisisitiza Mhandisi Kijazi.
Akifafanua,
Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa
la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika
kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi
ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
yakuleta mageuzi makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma
zinazotolewa kwa wananchi.
Aliongeza
kuwa Kikao kazi hicho kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila
mwaka ili kuwapa fursa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala kubadilishana
uzoefu, kubaini changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa
kuzitatua kwa maslahi ya wanachi.
Akizungumzia
mabadiliko yaliyofanywa na Serikali Balozi Kijazi amesema kuwa ni
pamoja na kuwepo kwa muundo mpya kwa Wizara zote unaoendana na mahitaji
na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano utakowezesha kutatutuliwa kwa
changamoto zilizokuwepo kabla ikiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya
lazima.
Kauli
mbiu ya Kikao kazi hicho ni “Uongozi makini na wapamoja unaozingatia
uzalendo, uwajibikaji, utawalabora na kusimamia rasilimali zetu ni
nyenzo muhimu katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa Kati”
Alisisitiza Balozi Mhandisi Kijazi.
Kikao
Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara, Makatibu Tawala wa Mikoa Kinafanyika
Jijini Dodoma kwa siku tatu kikilenga kuimarisha na kuongeza tija
katika kuwahudumia wananchi kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akifungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Mtendaji Mkuuwa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akisistiza jambo wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya Makatibu Wakuu wakifuatilia uwasilisjhaji wa mada mbalimbali kwenye Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Bw. James Syanga akiwasilisha mada kuhusu athari za madawa ya kulevya wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Manaibu Katibu Wakuu na Makatibu Tawala wakifuatilia mada wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma. (Picha zote na Frank Shija- MAELEZO)
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi akijitambulisha wakati wa wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw. David Kafulila akijitambulisha wakati wa wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nichalaus William akijitambulisha katika kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu mara baada ya kufungua kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19,2018.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa mada wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018 wakiwemo Makatibu Wakuu.
No comments:
Post a Comment