HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 7, 2018

MAHAKIMU WAANDAMIZI WAPONGEZA ELIMU WALIYOIPATA KUHUSU SHERIA YA FIDIA KWA MFANYAKAZI

 Waheshimiwa Mashakimu Wakzi wa Mikoa na Wilaya kutoka Mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wakiwa kwenye mahakama ya mfano ili kujipima kuona uelewa wao kuhusu Sheria ya Bunge ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 5  [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] naada ya kushiriki mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na kuratibiwa kwa pamoja na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 5-6, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro


MAHAKIMU wakazi wafawidhi wa Mahakama za Mikoa na Wilaya kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wamefurahishwa na mafunzo ya kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] ambapo jukumu lake kubwa ni kutoa fidia kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.
Kutokana na jukumu hilo la Mfuko, Chuo cha Uongozi wa Mahama Lushoto ambacho ndicho chenye dhamana ya kutoa mafunzo kwa watumishi waandamizi wa mahakama, kiliandaa mafunzo hayo ili kuwawezesha viongozi hao wa mahakama wa ngazi za mikoa na wilaya kuelewa vema Sheria hiyo ili iwe rahisi kwa wao kutoa maamuzi sahihi endapo mashauri yahusuyo fidia kwa wafanyakazi na shughhuli za Mfuko yatafika mbele yao. Amesema Mkuu wa Huduma za Sheria wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Abraham Siyovelwa.
Wakizungumza katika mahojiano baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, alisema
“Nimefurahia sana kupata mafunzo haya, mimi nina nafasi mbili, kwanza kabisa kama mfanyakazi,  lakini pia kama mdau mkubwa wa Sheria ya Mfuko huu kama hakimu, nimefaidika sana na elimu hii kwani nimeelewa vitu vingi ambavyo hapo awali sikuwa nikivijua.”
Alisema, elimu aliyoipata kama mtumishi wa mahakama, ameelewa haki zake za msingi kuhusiana na Mfuko huo wa Fidia ameridhika na kufurahia kuwa anafanya kazi katika mazingira ya uhakika na akiamini pia hata wategemezi wake lolote likimtokea kutegemea na Mungu amepanga nini, basi wategemezi wake wanaweza kunufaika licha ya yeye mwenyewe.
“Uelewa nilioupata baada ya mafunzo haya ni mkubwa sana hususan kwenye makosa ya jinai yameelezwa bayana, na nimeelewa jinsi nitakavyosimamia sheria hii endapo nitakutana na kesi yoyote itakayoletwa mbele yangu, kwa sababu ninailewe sheria hii kwa kina.” Alisema
Alishauri pia Mfuko uendelee kutoa elimu hususan kwa wafanyakazi, kwani wengi hawajui manufaa ya huu Mfuko.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi, Mhe. James Mutakyahwa Karayemaha amesema, mafunzo aliyoyapata yamemfanya apate uelewa mpana kuhusu sio tu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na namna gani anapaswa kuisimamia wakati atakapokutana na mashauri yahusuyo Fidia kwa wafanyakazi, lakini pia amepata uelewa wa faida anazoweza kupata yeye binafsi kama mtumishi wa umma.
“Nimejua kuwa mwajiri kwa mujibu wa Sheria hii, anao wajibu wa kujisajili na kuwasilisha michango ya kila mwezi kwa Mfuko na asipofanya hivyo anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo,  faini au vyote viwili.” Alisema
Alisema pia amejua kuwa kama mfanyakazi hapaswi kushwishiwa kwa namna yoyote ile na mwajiri wake, kutoa taarifa mbili tofauti za viwango vya mishahara, ambapo taarifa za malipo ya mtumishi zikionyesha kiwango cha juu cha mshahara na taarifa zinazopelekwa WCF zikionyesha kiwango cha chini cha mshahara.
“Taarifa hizi zisizosahihi kama hizi ni janga kwa mfanyakazi kwani endapo atapatwa na tatizo lolote la kuumia akiwa, kuugua au hata kifo akiwa kazini, inapofika wakati wa kufidiwa, malipo hayo yatazingatia taarifa za malipo ya mshahara zilizokuwa zikiwasilishwa  kwenye Mfuko.” Alisema.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara, Mhe.Godfrey Mwambapa, alisema kimsingi yeye ameongeza weledi kuhusu sheria inayoendesha na musimamia shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
“Mfuko huu nunatuhusu watu wote tulio kwenye ajira na kwakweli unatusaidia hasa kuwa salama sehemu ya kazi endapo utapatwa na matatizo sehemu ya kazi Mfuko huu utakuja na kunifanya niishi kama vile nikiwa kazini na kuniondolea magumu yote ya kimaisha.” Alsiema.
Alisema, yeye kama hakimu ameweza kuelewa sheria inayosimamia Mfuko na hata kama shauri lihusulo masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi litamfikia mbele yake yuko katika nafasi nzuri ya kusimamia sheria hii kwani ameielewa vilivyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, mafunzo hayo ni muendelezo wa mipango ya Mfuko kutoa elimu kwa wadau wote ambapo tayari Mfuko umetoa elimu kw amadaktari kote nchini, Waajiri kote nchini, lakini pia elimu kwa wafanyakazi kwenye maeneo yao ya kazi kupitia ziara za maafisa wa WCF kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini.

 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Chuom cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, (IJA), Mhe. jaji Dkt.Paul Kihwelo, akitoa nasaha zake kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya JIA na WCF. Aliyesimama kushoto ni mratibu wa mafunzo, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo hicho, Mhe. Lameck Samson.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Temeke jijini Dar es Salaam, Mhe. Susan P. Kihawe (kuli) akifurahia jambo wakati akizungumza na mwenzake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ilala, Mhe. Martha Mpaze.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, akizungumza.

 Waheshimiwa mahakimu wakiwa kwenye majadiliano ya vikundi.
 Mhe.S.Mwalusamba (kushoto) na Mhe.Godfrey Mwambapa wakifuatilia kwa makini.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Mhe. Gofrey Isaya, akizungumza
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Pwani, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Mhe. Batista Kashushe, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Mhadhiri Msaidizi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Lameck Samson akifafanua jambo.
 Hakimu Mkazi wa Mfawidhi Mahakama ya Kilombero/Ifakara Mkoani Morogoro, Mhe. L.Khamsini akisikiklzia kwa makini wakati Mkuu wa Huduma za Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada.
 Majadiliano ya vikundi
 Majadiliano ya vikundi
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (wapili kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka, mwishoni mwa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo mahakimu wakazi wa mikoa na wilaya yaliyofikia kilele mkoani Morogoro Septemba 6, 2018. Wengine pichani ni Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa. na kulia ni Mhadhiri Msaidizi, Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Lameck Samson.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (kulia) na Mkuu wa Huduma za Sheria, wa Mfuko huo, Bw. Abraham Siyovelwa, wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kuwapongeza mahakimu hao baada ya kumaliza mafunzo.
 Majadiliano ya vikundi.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), na Afisa Sheria wa Mfuko huo, Bw. Deo Victor wakijadiliana jambo mwishoni mwa mafunzo hayo.


Afisa Sheria WCF, Bw. Deo Victor (aliyesimama kulia) akisimamia majadiliano ya vikundi kuhusu kile kilichofundihswa. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad