HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 September 2018

KWESE IFLIX KURUSHA MICHUANO MIKALI YA NDONDI, WATEJA KUSHUHUDIA KUPITIA SIMU ZA MKONONI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

KUELEKEA michuano mikali ya ndondi kati ya Anthony Joshua raia wa Nigeria na mshindi wa mataji 3 yakiwemo ya WBA dhidi ya Alexander Povetkin kutoka Urusi watakao zichapa Septemba 22 Kwese Iflix kupitia application yao watarusha mpambano huo moja kwa moja kutoka katika viwanja vya Wembley kwa gharama nafuu ya shilingi 1300 pekee.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mkuu wa Kwese Iflix Mayur  Patel ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Kwese Iflix miezi mitatu iliyopita malengo yao ya kuendelea kutimiza haja ya burudani kwa wateja wao imezidi kuimarika kwani wateja wao hutizama masuala ya burudani za kila namna kupitia simu zao za mkononi na upeperushaji huo huwa ni wa moja kwa moja ukienda sambamba na uchambuzi wa kina hasa katika kabumbu.

Ameeleza kuwa pamoja na ndondi pia mashabiki wa mpira watafurahia michuano ya kimataifa ya UEFA Nations League inayoendelea moja kwa moja sambamba na uchambuzi kutoka kwa wabobezi wa masuala la mpira.

Aidha imeelezwa kuwa kwese Iflix ina huduma pana ya maktaba ya vipindi na filamu kutoka ndani na nje ya bara la Afrika kwa kushirikiana na zaidi ya studio 240 na wasambazaji wa filamu ulimwenguni, na hupatikana kwa  kujinunulia VIP pass itakayodumu kwa muda wa siku 1, 3, 7 hadi siku 30 na kwa kukamilisha hii ni kwa kupakua bure application ya Kwese Iflix kupitia Google na apple app store.

Fursa ya kurusha michuano hiyo imekuja baada ya Kwese Iflix kufanikisha urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya kombe la dunia mwaka 2018 kwa ufanisi zaidi.

Pia katika kuelekea pambano hilo la ndondi Kwese Iflix itatoa vidokezo na marudio ya makabiliano manne ya mwisho bure kabisa bila malipo na hasa yale ya ushindi kwa wateja wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad