HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 4 September 2018

KOCHA WA RIADHA AAHIDI MEDALI MASHINDANO YA TAIFA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Riadha Iddi Muhunzi 'kipepe' amesema vijana aliokuwa nao katika mazoezi yake kwa sasa wana uhakika wa kuleta medali kwenye mashindano ya Taifa yatakayoanyika baadae mwaka huu.

Akizungumzia maadalizi ya mashindano mbalimbali yanayotarajiwa kufanyika hapo baadae, Muhunzi amesema wataanza na kutafuta ya mkoa wa Dar es salaam na kutakuwa na mashindano ya wazi siku ya Jumamosi yatakayofanyika Uwanja wa Taifa ili kuwapata vijana watakaowakilisha mkoa.

Muhunzi amesema baada ya hapo watajiandaa na mashindano ya Namtumbo ya Half Marathon yatakayoshirikisha vijana mbalimbali na mpaka sasa vijana wana ari ya hali ya juu kuweza kufanya vijana vizuri.

Ameeleza kuwa, mashindano ya Taifa  anataka kuhakikisha vijana wake wanabakisha medali kutokana na morali kubwa waliyonayo na kutaka kufanya vizuri kwenye mashindano hayo wakianza katika mazoezi ya kila siku yanayoendelea.

Muhunzi amesema, amekuwa na hamasa kubwa sana kwa vijana hao na wengi wameonesha wana vipaji vikubwa vya kuja kuipatia medali taifa siku zijazo.

'Programu ninazowapatia ni za kufa mtu na wengi wameonesha moyo wa kujituma na kufanya mazoezi kwa nguvu zote na hilo limeonesha kuwa vijana wamedhamiria kuleta medali,'amesema Muhunzi.


"Kwa hamasa hii ya vijana inaonesha natumia vyeti vyangu vizuri sio kusomea halafu kujaza makaratasi ndani na hili litakuja kusaidia kupata vijana wenye vipaji vikubwa sana
'

Timu ya taifa ya riadha wanaendelea na mazoezi kwa sasa wakiwa wanajiandaa na mashindano mbalimbali yanayokuja hapo baadae na maandalizi yao yanaanzia siku ya Jumamosi kwa kuanza mashindano ya wazi ya kupata timu itakayowakilisha mkoa wa Dar es salaam na kisha mashindano ya Namtumbo kabla ya  kuanza kwa mashindano ya taifa.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad