HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 11 September 2018

EMIRATES WAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio na jinsi wanavyoliendesha shirika hilo. Pembeni ni mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, Tununu Kasambala. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwandishi wa TBC1 Stanley Ganzel akiuliza swali. Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania (hayupo pichani).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer (wa sita kutoka kushoto) akiwa na wanahabari waliohudhuria mkutano wake.

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer amesisitiza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wanaosafiri na ndege zao katika mataifa mbalimbali duniani.

Pia amezungumzia fursa zilizopo kutokana na uwepo wa safari za ndege zinazofanywa na Emirates kati ya Tanzania na nchi nyingine ikiwemo ya usafirishaji mizigo ya kibiashara kutoka Dar es Salaam ambako kumekuwa kituo kikubwa cha kibiashara kwa Afrika Mashariki.

Alfajeer amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari katika mazungumzo yaliyolenga kujenga uhusiano kati yake na vyombo vya habari kuhusu masuala ya kibashara na maisha.

“Emirates nia yetu ni kuendelea kuhakikisha wateja wetu wanakuwa wenye thamani bora kadri inavyowezekana,” amesema.

Hivyo wanaendelea kuwa wabunifu katika kutoa huduma bora zaidi. “Kila siku tumekuwa tukiangalia njia za ubunifu ili kuboresha huduma zetu kwa wateja ikiwa pamoja na kurahisi safari zao kati ya eneo moja ya jingine.”

Kuhusu mizigo amesema mingi kupitia Emirates kuna mizigo mingi ambayo inasafirishwa kutoka Dar es Salaam.

“Wapo wanaosafirisha nyama ya mbuzi, kondoo na dagaa kutoka Tanzania. Hivyo uwepo wetu umetoa fursa za kiabishara,” amesisitiza.

Pia Alfajeer amesisitiza wanayo mikakati ya kuhakikisha wanaendelea kujiimarisha kibiashara.” Mkakati wa biashara wa Emirates daima tunazingatia fursa za biashara,” amefafanua.

Amezungumzia huduma za kipekee wanazozitoa kwa wateja wao. “Wakati wa safari wateja wetu wanapata vyakula vilivyo bora huku wakipata burudani za aina mbalimbali .

“Kwa watoto wanasafiri na Emirates nao tumezingatiwa mahitahi yao yakiwamo ya kuangalia game wakati wa safari.

“Pia mahitaji ya chakula kwa watoto wenye umri kati ya umri wa miaka 2 na 12 yanapatikana ndege za Emirates,” amesema.

Ameongeza kuwa “Menyu ya chakula inahusisha mapendekezo ya watoto ikiwa ni pamoja na chaguzi za mboga”.

Pamoja na mikakati yao ya kibiashara ameahidi wataendelea kushirikiana na Tanzania ili kuongeza uzoefu wa kibiashara.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad