HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 12, 2018

Dk Mengi ataka watanzania kujiamini ujasiriamali

 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akizungumza na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mafunzo wa Asasi ya EO tawi la Tanzania, Bi. Miranda Naiman.
 Mmoja wa wajasiriamali hao ambao ni wamiliki wa makampuni  mbalimbali nchini akiuliza swali kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akisiliza kwa makini maswali kutoka kwa wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania (hawapo pichani), waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam.
 Wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, wakimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) alipokuwa akiwasimulia uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akitia saini nakala za kitabu chake ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ zilizonunuliwa na wajasiriamali hao ambao ni wamiliki wa makampuni  mbalimbali nchini mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika hoteli ya Coral Beach-Masaki, jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi katika picha ya pamoja na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania huku wakiwa wameshika nakala za kitabu chake ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika hoteli ya Coral Beach-Masaki, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Asasi ya Entrepreneurs Organization (EO) tawi la Tanzania Bw. R.J. Katunda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupata nasaha kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi (hayupo pichani) katika mkutano mfupi ulioandaliwa na Asasi hiyo Hoteli ya Coral Beach-Masaki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi katika picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania mara baada ya kupata nasaha kutoka kwa IPP Dk. Mengi katika mkutano ulioandaliwa na Asasi hiyo Hoteli ya Coral Beach-Masaki jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Wajasiriamali nchini wametakiwa kujiamini kuwa wanaweza kuletea maendeleo kwa kugundua na kutumia ipasavyo fursa za uwekezaji zilizopo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi kwenye mazungumzo na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga.
Amesema Watanzania hawana budi wajiamini kuwa kwa jitihada zao wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwekeza kwenye fursa anuwai  zilizopo nchini, wakati huu ambapo Rais John Magufuli anahamasisha uwekezaji, hususan  wa viwanda, baada ya kuboresha mazingira ya uwekezaji.
Alisema hilo linawezekana kwa kujifunza kusema kwamba nitaweza na lazima na kisha kutekeleza uthubutu huo kivitendo.
Alisema kwamba yeye akiwa anatoka katika familia maskini aliweza kufanikisha kuwa mfanyabiashara mkubwa kutokana na dhamira yake ya kusema nitaweza na kutekeleza msemo huo kwa vitendo.
Aidha alisema aliandika kitabu hicho kama alivyoshauriwa na mtoto wake Rodney ili kuwashawishi watanzania wengi zaidi kuwa na uthubutu na ushauri katika kujikita kwenye ujasiriamali na kutumia fursa.
Aidha aliwataka watanzania kujifunza na kuwa wabunifu na watunga sera kuona kama elimu yetu ya sasa inakidhi mahitaji halisi au inatakiwa kuboreshwa ili kusaidia katika harakati za kuipeleka nchi yetu kwenye uchumi wa kati.
Alisema hayo wakati akijibu maswali katika mdahalo huo kuhusu elimu na kama elimu yetu inafaa kwa sasa.
 Alisema kitabu alichotunga kinaelezea uzoefu wake katika ujasiriamali kutokana na ukweli kuwa hata wakati wa kuanzisha IPP ni kuwezesha ubunifu na teknolojia miongoni mwa watanzania.
Wakati wa mazungumzo hayo yaliyosimamiwa na Mwenyekiti wa Mafunzo Bi. Miranda Naiman, Dk Mengi pia alipata fursa ya kutia saini yake nakala za kitabu chake zilizonunuliwa na wajasiriamali hao ambao ni wamiliki wa makampuni  mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Asasi ya Entrepreneurs Organization (EO) tawi la Tanzania Bw. R.J. Katunda amesema ni jambo la kawaida kwa asasi  hiyo ya kimataifa tawi la Tanzania kuwaalika watu mashuhuri ili kujifunza kutoka kwao.
Alisema ni kitu chema kuchota maarifa kutoka kwa wazee kama Mzee Mengi .
Alisema mkutano wao ulikuwa wa maana sana kutokana na Dk Mengi kuchambua kitabu chake na kueleza uzoefu wake miongoni mwa kundi hilo lenye wajasiriamali vijana.
Katunda alisema taasisi hiyo ya wajasiriamali ilianzishwa nchini Tanzania mwaka 2015 na kila mwezi hukutana kupata maarifa zaidi ya kuendesha makampuni yao na hapa nchini wapo wanachama 30.
Alisema EO ina wanachama 13,000 katika makundi 160 (Chapter) na Tanzania ikiwamo.
Alisema pamoja na kuwaita wazee mbalimbali pia wamekuwa na nafasi ya kuwaita wakufunzi kutoka katika taasisi yao makao makuu ili kuwanoa katika nyanja mbalimbali za ujasiriamali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad