HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 15, 2018

DC Chongolo aomba taarifa uharibifu wa Mto Tegeta

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ameuagiza  uongozi wa bonde la Mto Wami/Ruvu kupeleka taarifa ya uchafuzi wa mto Tegeta lililoathiriwa na shughuli za Binadamu.
Chongolo aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika bonde la Mto Tegeta eneo la Salasala, amesema uharibifu ni mkubwa kwa shughuli za kibinadamu ambapo ni hatari kwa wananchi wa liopo kandokando ya Mto huo.
Amesema kuwa hakuna sababu ya kuacha uharibifu mazingira wakati vyombo vya kusimamia vipo.
Chongolo amesema wananchi lazima waheshimu sheria zilizowekwa katika bonde mabonde ya Mito.
"Hatuweza watu wakaendelea kuchimba mchanga huku wakiharibu mazingira na baadae serikali kuingia gharama ya kuhudumia wananchi waliohadhilika na mafuriko wakati shughuli za uchimbaji mchanga  walizifanya wenyewe"amesema Chongolo.
Nae Afisa wa Maji wa Bonde la Mto wa Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa watu kama wanachimba mchanga lazima wafuate utaratibu.
Amesema kuwa hakuna sababu ya kuacha uchimbaji wa mchanga wa holela na kama hawataki kufuata sheria waache kuchimba mchanga katika mabonde ya Mito.
Amesema kuwa kuna operesheni wataifanya hakuna mtu atabaki salama kwa wachimbaji wa mchanga.
Aidha amesema kuwa wachimbaji  wa mchanga lazima waheshimu sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad