HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 7 September 2018

DC ahimiza jamii za wafugaji kusomesha watoto wa kike hadi chuo kikuu

Na Ahmed Mahmoud Simanjiro
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula amezitaka jamii za wafugaji kuanza kuchukua hatua dhidi ya Mila potofu zinazoendelea kumkandamiza Uhuru wa mtoto wa kike na kumfanya ashindwe kusoma kwa maslahi ya wazazi wake

Aidha ameitaka jamii hiyo ya kabila la kimasai kubadilika na kuanza kusomesha watoto wa kike hadi vyuo vikuu ili kuwapatia elimu itakayosaidia kuielimisha jamii hiyo ili kuachana na mila potofu zikiwemo ndoa za utotoni na ukeketaji .

Kauli hiyo ameitoa mapema jana katika kijiji cha Namalulu,wilayani Simanjiro,Mkoa wa Manyara wakati  alipohudhulia   sherehe za Kimika za kusimikwa kwa viongozi wakuu wa kabila la Kimasai alimaarufu Laigwanani.,Ambapo  Mzee Meshack Toreto na Lucas Kisongira walisimikwa kuwa viongozi wakuu wa Kimila katika jamii hiyo.

"Jamii za kifugaji lazima zianze sasa kumwandaa mtoto wa kike kwa ajili ya kumpatia Elimu bora ili aje kuikomboa jamii hiyo ambayo baadhi yao bado wanaendekeza mila potofu zilizopitwa na wakati''Amesema chaula

Mhandisi Chaula alisema serikali inaunga mkono mila na destuli za makabila mbalimbali na aliahidi kushirikiana na viongozi wa kimila  na kuwataka kufuata taratibu na sheria za nchi ikiwemo kuhamasisha maendeleo na kujiepusha na tamaduni zinazokinzana na sheria za nchi.

Ameipongeza jamii huyo ya kimasai kwa  hatua hiyo ya kuendelea kudumisha mila na tamaduni zao jambo linaloendelea kulipa sifa taifa katika nyanja za kimataifa kwani kwa hapa nchini ni kabila pekee linalotambulika kimataifa katika utamaduni wao unaoleta tija kimataifa.

Awali katibu wa viongozi wa kimila Ilaigwanak, Mchungaji Yohana ole Tiamongoi amesema kupitia viongozi hao wa kimila wamefanikiwa kuziondoa mila mbalimbali potofu katika jamii yao kupitia maadhimio mbalimbali kwenye vikao vyao.

Katika sherehe hizo za kusimikwa viongozi hao wa kimila katibu huyo amewataka wafugaji wa jamii hiyo kuanza kuwekeza kwa mtoto wa kike kwa kumpatia Elimu hadi  chuo kikuu.

Mmoja wa Laigwanani aliyesimikwa ,Meshack Toreto alisema kuwa kazi yao kubwa ni kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii yao ikiwemo migogoro ya Ardhi ili kuisaidia serikali kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani yanayotokana na migogoro ya jamii hiyo.

"Sisi hatupingi watu wetu kwenda kwenye vyombo vya kisheria ila tunataka zaidi mambo yetu kuyamalize wenyewe na hii itasaidia hata serikali kupunguza mzigo wa wa kuendesha kesi mahakamani''Amesema Toreto

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula (kushoto) akimkabidhi rungu maalumu mmoja ya wazee wakubwa, Meshack Toreto aliyesimikwa kuwa Laigwanani wa kabila la wamasai katika kijiji cha Namalulu, wilayani Simanjiro jana.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad