Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni ambaye ni
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
-TPSF Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi ya
wageni waalikwa mara baada ya kuwasili kwenye tafrija ya maazimisho ya
Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Tanzania Bw. Gift Shoko na wa pili
kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya CBA nchini, Bw. Vinoo Somaiya na mmoja
wa wageni waalikwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko
akikamkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni
ambaye ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi kwenye eneo maalum walipomuandalia
wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu
kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji anayeshughulikia Masoko
Makao Makuu ya Benki ya CBA, Chris Pasha na Wa pili kushoto ni Mkuu wa
Huduma za Kibenki na Masoko wa benki ya CBA nchini, Julius Konyani.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (katikati)
akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Benki ya CBA nchini Vinoo Somaiya
(kulia) wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka
10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa
Benki ya CBA, Martin Mugambi.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni ambaye ni
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
-TPSF Dk. Reginald Mengi akizungumza na wageni waalikwa pamoja na
wafanyakazi wa benki ya CBA (hawapo pichani) wakati wa tafrija ya
maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa
nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi akitoa salamu
za benki hiyo kwa wageni waalikwa pamoja na mgeni rasmi (hawapo pichani)
wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu
kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko akizungumza
na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa tafrija
ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake
hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mmoja wateja wa Benki ya CBA nchini, Allan Makame akitoa ushuhuda jinsi
alivyofanikiwa kibiashara kutokana na mikopo yenye gharama nafuu
inayotolewa na benki hiyo wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo
kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris
Mollel akizungumzia kazi za taasisi yake kabla ya kuendesha mnada wa
vitu ili kuchangisha fedha za kusaidia watoto njiti katika hospitali ya
wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, ambapo jumla ya shilingi milioni 17.6
zilipatikana wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Huduma za Kibenki na Masoko wa benki ya CBA nchini, Bw. Julius
Konyani akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa (hawapo pichani)
wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu
kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Taasisi ya Doris Mollel Foundation ikiendesha mnada wa vitu ili
kuchangisha fedha za kusaidia watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya
Same Mkoani Kilimanjaro, ambapo jumla ya shilingi milioni 17.6
zilipatikana wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa nchini iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugeni wa Benki ya CBA, Suzane Ndomba akikabidhi zawadi kwa mmoja wa
wateja aliyeshiriki mchezo wa gofu katika kusheherekea maazimisho ya
benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mtendaji anayeshughulikia Masoko Makao Makuu ya Benki ya CBA, Chris
Pasha (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi wa mchezo wa
gofi katika katika kusheherekea maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka
10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk.
Reginald Mengi (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA,
Martin Mugambi wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa
gofu kutoka Zambia wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA
kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk.
Reginald Mengi katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa tafrija ya
maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa
nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Elias Barnaba 'Barnaba Classic' akitoa
burudani ya wimbo maalum wa kupongeza benki ya hiyo tafrija ya kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa benki ya CBA wakicheza
‘kwaito’ wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka
10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria
tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa
kwake tena hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris
Mollel akizungumza jambo na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa tafrija
ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake
hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi katika picha ya
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa tafrija ya
maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa
nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk.
Reginald Mengi ( wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko (kushoto),
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi (wa pili kulia)
pamoja na Mkuu wa Mauzo na Huduma Binafsi za Kibenki wa benki ya CBA
nchini Bi. Edditrice Temba.
Mkuu wa Huduma za Kibenki na Masoko wa benki ya CBA nchini, Bw. Julius
Konyani (katikati), Mkuu wa Mauzo na Huduma Binafsi za Kibenki wa benki
ya CBA nchini Bi. Edditrice Temba pamoja na Mkuu wa kitengo cha Remedial
wa benki ya CBA nchini Bi. Queen Siraki (kushoto) katika picha ya
pamoja wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10
tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CBA nchini katika picha ya pamoja wakati wa wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ameitaka benki ya biashara ya CBA kuendelea kuwawezesha watanzania, hususani wa chini wapatao milioni 7.5 kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Dk. Mengi alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo mjini Dar es salaam ambapo yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Pamoja na historia ndefu ya benki hiyo ilivyoanzishwa na baadae kuhamishia makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, Dk. Mengi alisema benki hiyo ina wajibu mkubwa wa kuwezesha kundi kubwa la watanzania kuukataa umaskini.
Dk. Mengi ambaye ametoa kitabu kinachoonesha jinsi ya kukabiliana na umaskini na ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF, amesema amevutiwa na mpango wa Benki hiyo wa kuwapatia mikopo watu wa kawaida sana kupitia mpango wake wa kuweka akiba kupitia simu za mikononi ujulikanao kama M- Pawa.
Alisema anaamini kama benki imedhamiria na kujiamini wanaweza kujipatia mafanikio makubwa kupitia falsafa ya ninaweza. Anasema njia ya dhamira ya kwamba mtu anaweza hakuna cha maana kinachoweza kufanyika.
Mapema viongozi mbalimbali na waalikwa wakizungumzia huduma ya CBA tawi la Tanzania walisema kwamba inawasaidia sana hasa watu wa kipato cha chini na hivyo wanajihakikishia maendeleo kupitia M-pawa.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Martin Mugambi, na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Tanzania Bw. Gift Shoko walisema benki ya CBA yenye umri wa miaka 56 barani Afrika ina wateja zaidi ya milioni 35, na hapa nchini imewekeza mtaji wa dola za kimarekani milioni 50.
Viongozi hao wawili walisema kwa msisitizo mkubwa wanatoa huduma bora zinazounganisha wananchi katika kupata mikopo na kuweka akiba.
Walisema kwamba mipango yao ni kuimarisha huduma za wateja wadogo kwa kuwa wao ndio tegemeo la kuinua uchumi wa Tanzania kupitia ujasirimali.
Tafrija ya Maadhimisho hayo ilipambwa na mnada ulioendeshwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation, wa kuchangisha fedha za kusaidia watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, ambapo jumla ya shilingi milioni 17.6 zilipatikana.
No comments:
Post a Comment