HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 11 September 2018

BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI

Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MSIMU wa Tisa wa mashindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS) umezinduliwa rasmi ikishirikiana na Kampuni ya Startimes jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wanahabari Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wanawapongeza BSS kwa kukuza vipaji toka msimu wa kwanza mpaka msimu huu ujao ambao unatarajia kuruka hewani hivi karibuni kupitia Startimes Swahili .

Malisa ameeleza mipango yao kushirikiana na Bss kuhakikisha inakuza vipaji na kunyanyua vijana kuonyesha vipaji vyao,  pia kipindi hiki ni chenye maudhui na kinaweza kutazamwa na rika zote .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark production ambae pia ni Jaji Mkuu Ritta Paulsen ameiomba Serikali kuangalia na kutoa mchango kwenye sekta ya muziki kwani inaongeza Pato la Taifa na wasanii wamekua wakiendesha maisha yao kupitia muziki.

Hivyo  amesema katika  msimu huu wanaomba ushirikiano kwa watanzania wote kwani wanaamini hiki ni kipindi kinachofatiliwa na watu wengi sana kwa hiyo vijana wajitokeze kuonyesha vipaji vyao.

Kuhusu ratiba ya usahili itakua mikoa mbalimbali kamaMwanza, Dar es salaam,  Arusha, Mbeya na usahili huo utaanza  Septemba na kauli mbiu ikiwa ni Jiongeze piga hatua.

Wakati huo huo mmoja wa wasanii ambao wameibuka baada ya kuibuliwa na  BSS  Kala Jeremaya amewapongeza Benchmark kwa kulirudisha shindano hilo na kueleza mafanikio ambayo amepata.

Amesema  kwani amekua akishirikiana na watu wakubwa kutoka mashirika mbalimbali kutokana na fursa ambayo amepata kutoka kwenye shindano na kumtambulisha vizuri na kumpa fursa kujulikana kwa urahisi zaidi huku akiendesha maisha yake kupitia muziki wake.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisaakizungumza na waadishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Majaji wa shindano hilo wakifurahia jambo
Uongozi wa Startimes Tanzania pamoja na  uongozi wa Bongo Star Search wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa
shindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad