HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

BEN POL AACHIA NGOMA MPYA YA NTALA NAWE AKIMSHIRIKISHA MSANII KUTOKA KENYA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya nchini Bernard Paul 'Ben Pol' ameachia wimbo mpya unaoitwa Ntala Nawe ukiwa  umetengenezwa nchini Kenya chini ya mtayarishaji Cedo. 

 Akizungumza Dar es Salaam, Ben Pol alisema kuwa wimbo huo umetoka kwa Audio na Video ambayo imefanywa hapa nchini na mtayarishaji Hanscana, huku msanii wa filamu Monalisa akiwa muongozaji wake.

 Alisema kuwa tayari Ntala nawe imeshaingia mtaani kwa kusambaza katika vituo mbali mbali vya Televisheni na Radio.

"Mashabiki wangu nimekuja tena na wimbo mpya unaitwa Ntala Nawe naamini mnaoupokea na kuupenda kama nyingine zilizopita, tayari upo YouTube kwa wale wanaopenda kuangalia video na kusikiliza"alisema Ben Pol.. 

 Alisema katika wimbo huo amemshirikisha Cedo kutoka nchini Kenya,  na kwa sasa Ben Pol amekuwa akitamba kwa nyimbo mbalimbali ikiwepo Sofia, Phone, Samboira, Lau nipe nafasi, Gusa na Bado Kidogo pamoja na wimbo wa Amen alioshirikiana na mwanadada Maua Sama.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad