HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 25 September 2018

AZAM MEDIA WACHANGIA MILIONI 5 KWA AJILI YA KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amepokea kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000) kutoka kwa uongozi wa Azam Media wakichangia katika kampeni ya Tokomeza Zero.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tdo Mhando amesema kuwa wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ya kuhamasisha wananchi kuchangia ili kutokomeza Zero kwenye Wilaya hiyo.

Tido amesema kuwa, wao kama uongozi wa Azam wanachangia kiasi ch Milioni tano (5,000,000) ili kusaidia kampeni hiyo na bado wataendelea kushirikiana katika nyanja zingine za kimaendeleo kwani huu ni mwanzo.

Baada ya kupokea hundi ya Kiasi hicho, Mkuu wa Wilaya Jokate amewashukuru uongozi wa Azam kwa kuweza kuona umhimu wa kuungana nae kwa kushirikiana  na kumpatia kiasi hicho kitakachowasaidia kuhakikisha wanafunzi wanapata mahitaji yote kwenye kipindi hiki kuelekea mtihani wa kidato cha nne.

Jokate amesema wanafunzi wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wananchi mbalimbali kwa kiasi chochote walichonacho ikiwemo mahitaji muhimu kama unga, sabuni, mafuta na kadhalika, kwani katika kipindi hiki wapo wamekaa mahali wanajisomea na vitu vinavyopatikana vinawasaidia wao.

Amesema kwua, wanafunzi hao kwa sasa wanahudumiwa na serikali ya Wilaya ya Kisarawe  chini ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Twala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye ni Mbunge  wa Kisarawe Seleimani Jaffo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando akimkabidhi mfano wa hundi ya Kiasi cha Shilingi Milioni tano (5,000,000) kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa ajili ya kampeni ya Tokomeza Zero.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad