HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 12 August 2018

WEZI WA MAJI YA DAWASCO WAKAMATWA TEMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limeendesha operesheni ya kuwakamata wale wote waliojiunganishia maji na mkufanya biashara ya maji bila ya kuwa na kibali. Akizungumza Kaimu Meneja wa DAWASCO mkoa wa Kimara, Frank Sulley amesema wameamua kuendelea na operesheni yao maana watu hao wamekuwa wakihujumu shirika hilo kwa kuiba maji huku wakiharibu miundo mbinu. 

"Tupo eneo la Kimara Temboni na tumewamata mama (jina kapuni) ambaye alikuw akifanya biashara ya maji na kuharibu miundo mbinu, kwa kukata bomba na kujaza tanki lake na kufanya biashara ya kuuza maji ambapo amekuwa akiuza tsh 6,000 kwa tanki la lita 1,000,' amesema Sulley. 

Amesema kuwa kumekuwa na mchezo wa kujiunganishia maji kwa njia ya kinyemela kwa kukata bomba nyuma ya mita na kutumia huku mita ikiwa haisomi jambo linalohujumu uchumi wa shirika hilo. Aliongeza kuwa amewataka wateja kujitokeza kujisalimisha wale wote waliojiunganishia kinyemela kabla ya muda haujaisha. Wafanyakazi wa DAWASCO wakifukua shimo kuweza kupaini jinsi uunganishani wa maji kinyemela ulivyofanywa na mkazi wa Kimata Temboni jijini Dar es Salaam wakati wa oparesheni ya kuwabaisni wanaofanya biashara ya maji kinyemela iliyofanyika mapema. Kaimu Meneja wa DAWASCO mkoa wa Kimara, Frank Sulley akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi stali mpya ya wizi wa maji unavyofanyika jijini Dar es Salaam.
Moja ya Tanki la maji lilipo ardhini linalotumika katika wizi wa maji na kuwauzia watu wa magari makubwa (maboza).
Moja ya muunganiko wa maji mabomba ya maji unaopeleka maji kwenye tanki. 
Gari hili lilikutwa eneo la tukio likijiandaa kupandisha maji na kuenda kusambaza kwa wateja, ambapo wao wamekuwa wakinunua maji kwa tsh 6,000 kwa tanki la lita 1,000 na kwenda kuliuza mtaani kwa tsh 12,00-15,000/- 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad