WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga(CCM) kulia akimkabidhi
madawati 40 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga
Daudi Nchia ikiwa ni mkakati wake wa kukabiliana na uhaba uliopo
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga(CCM) kushoto akiwa amekaa
kwenye moja ya madawati 40 aliyokabidhi kwa shule ya Sekondari Toledo
Jijini Tanga
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga(CCM) katika akiwa na Mwalimu
Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia mara baada ya kuwakabidhi
madawati 40
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga(CCM) akiwa kwenye picha ya
pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Toledo mara baada ya
kuwakabidhi madawati 40
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
WAZAZI kote nchini wametakiwa
kuacha kulalamikia wadau wa elimu na badala yake wameshauriwa
kushirikiana na walimu kukagua madaftari ya watoto wao kwa lengo la
kuongeza ufaulu ili kupunguza mimba za utotoni zinazosababisha ndoto
zao kushindwa kufikiwa.
Hayo yalisemwa NA Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati halfa ya
kukabidhiano ya madawati na viti vyake 40 aliyoyatoa kwenye shule ya
Sekondari Toledo ya Jijini Tanga.
Ummy ambaye ni Mbunge wa Viti
Maalumu kupitia chama cha Mapinduzi {CCM) mkoa wa Tanga alisema kimsingi
wazazi wanapaswa kutambua kufanya hivyo kutawasaidia kuwawezesha vijana
wao kuongeza ufaulu na hivyo kufanikiwa kuepukana na vishawishi ambavyo
wanakabiliana navyo wakati wakiwa shuleni.
“Ndugu zangu wazazi
na walezi lazima tutambue jukumu letu la kufuatilia maendeleo ya watoto
wetu kwani hii ndio njia pekee inayoweza kuwasaidia kwa kushirikiana na
walimu wao kwa lengo la kuwezesha kufikia ndoto zao”Alisema.
Naye
ka upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwataka
wanafunzi kutumia fursa hiyo kuongeza jitihada kwenye kusoma ili azma ya
serikali ya kuongeza ufaulu kwa shule zake iweze kufikiwa.
“Ndugu
zangu wanafunzi mmepata madawati haya yatumieni vizuri kwenye matumizi
yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yenu kwa
kuongeza ufaulu “Alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya
Sekondari Toledo Daudi Nchia alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo na
kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufu wa matundu ya vyoo vya wasichana .
Alisema
kutokana na uhaba huo umesababisha wasichana na wavulana kushiriki
katika huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment