HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 20 August 2018

WATANZANIA 20 WAULA WAPATA UFADHILI WA KUSOMA CHINA

Na Avila Kakingo,globu ya jamii.
KATIKA kukuza sekta ya mafuta na gesi hapa nchini serikali ya china yawapa ufadhili watanzania 20 kwenda nchini chini kusomea maswala ya mhimu ya gesi na mafuta ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza changamoto ya ukosefu rasilimali watu watakao simamia sekta hiyo.

 Akizungumza wakati wa kuwaaga watanzania hao 20 watakaoenda nchini china kusoma masuala ya mafuta na gesi, Katibu mkuu wa wizara ya nishati, Dk. Khamisi Mwinyimvua amesema kuwa wizara imekuwa ikidhamini watanzania kupitia serikali yawatu wa China katika fani ya mafuta na gesiipasavyo ili kutatua changamoto ya ukosefu wa lasilimaliwatu katika sekta hiyo.

“Kukua kwa sekta ndogo ya mafuta na gesi kumeleta changamoto ya upungufu wa rasilimali watu ya kusimamia sekta hiyo sasa wizara ya nishati ikishirikiana na serikali ya watu wa china imetoa ufadhili kwa watanzania 20 watakaoenda kusoma nchini China maswala ya mafuta na gesi, na leo tunawakabidhi barua za udahili.”

Mwinyimvua amesema kuwa serikalikupitia wizara ya Nishati na madini ilikubaliana na serikali ya watu wa china ili kutoa ufadhili huo wa masoma kwa fani ya mafuta na gesi kwa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu kwa watanzania kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano hadi 2019.

Pia amewaasa watanzania waliobahatika kuchaguliwa kupata ufadhili huo kutumia fursa hiyo vizuri kwa manufaa ya taifa kwa ujumla katika kuliwezesha taifa kutimiza malengo na dira ya maendeleo ya taifa katika sekta ya mafuta na gesi.
 Katibu mkuu wa wizara ya nishati, Dk. Khamisi Mwinyimvua (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwakabidhi watanzania 20 barua za udahili kwaajili ya kusoma nchini china jijini Dar es Salaam leo.
 Mwakilishi wa China nchini Tanzania akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya watanzania 20 watakaokwenda nchini china kusomea masuala ya mafuta na gesi  kwaajili ya maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi hapa nchini. Katibu mkuu wa wizara ya nishati, Dk. Khamisi Mwinyimvua akiwakabidhi barua za udahili kwaajili ya kwenda kusoma nchini China.Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam Agosti 20, 2018.

Picha ya pamoja.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad