HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 17 August 2018

WAMILIKI WA VING'AMUZI WATOA YA MOYONI, WAIPONGEZA TCRA KWA KUFUATA SHERIA,WATOA MSIMAMO

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAMILIKI wa visambusi(ving'amuzi)nchini wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusimamia na kufuata sheria.

Pia wameishukuru bodi ya TCRA na Mkurugenzi wake mkuu kwa kusimamia sheria dhidi ya waendeshaji wa PAY TV ambao wamevunja sheria kuanzia mwaka 2010

Wakizungumza jijini Dar es Salaam baadhi ya wamiliki hao wa visambusi wameanza kwa kueleza kwanini TCRA walitupatia leseni ya MUX (Multiplexer).

Pia kwa nini ilikuwa lazima kuanzisha mfumo wa watoa huduma kwa ving’amuzi (MUX) katika sekta ya matangazo ya luninga na nini lilikuwa lengo la lesseni hiyo?

Hivyo wamefafanua kuwa katika kipindi  baada ya mwaka 2000, vyombo vya udhibiti vilianza kupata tatizo la upungufu wa masafa (frequency).

Na kwamba hilo  lilikuwa tatizo la dunia nzima, ITU na wadau wake wakakubaliana kuhamia katika masafa ya kidigitali, katika mfumo wa kianalogia unahitaji frequency moja kwa chaneli moja ya TV.

Wakati katika mfumo wa kidigitali frequency moja inaweza kusafirisha kati ya chaneli 15-18 za Televisheni kupitia technologia ya DVB-T, au chaneli 20-25 kupitia teknologia ya DVB-T2 kwa kutumia teknologia ya kupunguza ya DVB-T na T2.

Pia katika mpangilio mpya, watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kutengeneza mtandao wa kusafirishia matangazo, na vituo vya televisheni vingetengeneaza maudhui ambayo yangebebwa na watoa huduma za ving’amuzi baada ya kukubaliana malipo.

Wamiliki hao wamesema watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kuweka miundombinu kama dishi, vifaa vya umeme, ama nyaya za kusafirisha matangazo kwa nje.

Pia Gharama za uwekaji wa miundombinu hutegemea ubora na chapa ya vifaa hivyo, mara nyingi inagharimu mamilioni ya dola za kimarekani kuweka miundombinu hii.

Wamesema kwa kuongezea, watoa huduma za ving’amuzi wanahitaji kuweka miundombinu ya kurushia matangazo katika kila mikoa, gharama ya mtambo mmoja unagharimu fedha nyingi sana.

Hivyo hasara walizopata kwa kuruhusu visimbusi vya kulipia kubeba chaneli za Bure

Wamefafanua hasara zinazohusiana na gharama za kurusha matangazo kutoka kwa watengeneza maudhui,suala la Visimbusi vya kulipia kubeba chaneli za bure (FTA) limeathiri mauzo ya ving’amuzi na kupungua kwa malipo ya kila mwezi.

Pia idadi waliyonayo wenye Visimbusi vya kulipia na tuliyonayo sisi vinashabihianaje?

Katika hilo wamejibu kwamba ni wazi kwamba wao kama Multiplexer, kwa pamoja wanavyo ving’amuzi vingi zaidi sokoni ukilinganisha na wale wenye huduma ya kulipia kama Azam, DSTV na ZUKU.

"Gharama waliyokuwa wanapata wenye vibali vya kurusha matangazo nchi nzima kabla ya kuhamia digitali, ukilinganisha na sasa baada ya kuhamia digitali," wamesema.

Wameongeza kabla ya kuhamia kwenye matangazo ya kidigitali, wataoa maudhui (Chaneli za luninga) kila mmoja wao alitakiwa kujenga na kufanyia matengenezo mfumo wake wa kurushia matangazo, gharama ambazo kwa sasa zinabebwa na sisi watoa huduma za visimbuzi (Multiplexer)

Hivyo  kwa njia hiyo vituo vya televisheni vinapunguza matumizi makubwa katika uendeshaji wake.

Pia mapato yatokanayo na matangazo ambayo wanapata huku wakiwabeba bila kulipia gharama za urushaji wa matangazo tangu mwaka 2010.

Wamiliki hao wamesema mapato yatokanayo na matangazo, kati ya vitu vingine yanategemea na ukubwa wa sehemu ambapo mawimbi yanafika (idadi ya ving’amuzi), kuwepo wa watoa maudhui wa chaneli za bure katika visimbuzi vitatu (Multiplexers) kunawasaidia sehemu kubwa katika majumba ya watu

",Hivyo tunakuwa tuewapatia jukwaa kubwa wanalohitaji kwa ajili ya kufanya biashara ya matangazo, matangazo ya biashara hayarusiwi kwenye visimbuzi vya kulipia hivyo ilkuwa ni kosa kwa chaneli za bure kuonekana kwenye visimbuzi vya kulipia.

"Baada ya kuhamia digitali, kwa sababu chaneli inaweza kurusha vipindi vingi zaidi vya ndani, hivyo ingesababisha kuongezeka kwa kiwango na ubora wa uzalishaji wa matangazo ili kuinua tasnia ya luninga," wamesema.

Wameongeza pia itakuwa maarufu na kupendwa kwenye miongoni mwa wananchi hivyo kupata watumiaji wengi zaidi.

Hivyo wamesema kiujumla ukitazama mabadiliko kuingia mfumo wa kidigitali kwenye nchi mbalimbali za ITU, mapato yatokanayo na matangazo ya biashara kwa tasnia nzima ya luninga yameongezeka kwa kiwango kikubwa.

Hivyo basi, kuanzia sasa  Chaneli ambayo haitalipia ila mtoa huduma ya maudhui anapaswa kuhakikisha kuwa Signal yake inayoletwa kwa waendeshaji wa MUX(warushaji wa matangazo) iko katika ubora.

Wamesena wanaweza kuweka ubora ambao tunapewa na watoaji huduma za maudhui(CSP).

Pia wanatoa  muda wa mwezi mmoja ambaye hatolipia ada za urushaji wa matangazo atakatiwa huduma mara moja.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad