HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 2 August 2018

Wadau waiomba serikali katika uwekezaji katika Lugha ya Kiswahili

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wadau wa elimu wameiomba serikali kuwekeza katika lugha ya kiswahili ili kiweza kufundisha wanafunzi na kuelewa pamoja kufaulu masomo kwa kutumia lugha hiyo.

Wakizungumza katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi ,Sekondari  na vyuo vikuu wamesema kunahitaji uwekezaji wa lugha ya kiswahili licha wanafunzi wanafaulu masomo yanayofundiahwa kiingereza kuliko somo la Kiswahili.

Mdahalo uliandaliwa na Haki Elimu kwa kushirikisha wadau namna ya lugha ya kiswahili kutumika katika kufundishia.

Akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Elimu Dk.John Kalage amesema kuwa mjadala huo ni muhimu kwa nchi katika kutathimini kwa kina nafasi ya lugha ya kiswahili ya kujifundishia na kujifunzia katika lengo la utoaji wa elimu nchini na dira ya nchi ya kuwa la Uchumi wa kati ifikapo 2025.

Amesma mdahalo huo ni kuishauri serikali katika kufikia mwafaka juu ya suala la lugha ya kiswahili kutumika katika kufundishia na kujifunzia.

Kalage amesema nyenzo muhimu katika maendeleo ya ustawi wa taifa lolote lugha ya kufundishia ndio nyenzo kubwa ya kuhamisha maarifa ,Stadi,Ujunzi na tamadini kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.

Kwa upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kandege amesema kiswahili kiwekezwe kama uwekezaji mingine katika nchi.
Amesema kuwa na lugha ya kiingereza kina umuhimu wake na sio kuacha kabisa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Haki Elimu, Dk. John Kalage akifungua mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuu  jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar as Salaam Dkt.Michael Kadeghe akiwasilisha  mada katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuu jijini Dar as Salaam.
 Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar as Salaam Profesa Martha Qorro akiwasilisha mada katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuu jijini Dar as Salaam.
Sehemu ya wadau mbalimbali  wa elimu  wakiwa katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuuuliofanyika jijini Dar as Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad