HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 29, 2018

VIONGOZI WAPYA WA TSA WATALETA MAENDELEO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema kuwa uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) ulienda vizuri ingawa kulikuwa na changamoto zilizojitokeza hapo awali.

Uchaguzi huo uliofanyika mapema wiki hii, uliweza kuwapata viongozi wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne ambao wameapa tayari kwa ajili ya kuanza kutumikia nafasi zao kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo.

Akizungumzia uchaguzi huo Afisa habari wa BMT Najaha Baklari amesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani kubwa sana ingawa awali kulitokea changamoto mbalimbali na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Juma Ikangaa aliweza kutoa rai kwa wagombea wote walioshinda nafasi zao wakazitumikie kwa ueweledi mkubwa ili kuleta manufaa kwa chama hicho, pia hata wale ambao hawakupata nafasi wae dele kuunga mkono.

Amesema kuwa  uchaguzi ulikuwa na ushindani mkubwa sana hususani katika nafasi za  Makamu Mwenyekiti  na Katibu Mkuu ambapo zilikuwa na wagombea zaidi ya mmoja na nafasi nyingine kuwa na mgombea mmoja mmoja lakini hakukuwa na wakati mgumu sana katika nafasi ya mwenyekiti, Mweka Hazina na Mkugenzi wa Elimu na Maendeleo ambazo  zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.

Katika uchaguzi huo, Imani Dominick alishinda kwa kupata kura 21 kati ya 26, Asmah Hilal alishinda  Makamu Mwenyekiti baada ya kumshinda kiongozi mzoefu , Thauriya Diria. Asmah alipata kura 19 na  Diria akipata kura saba (7).  Mgombea mwingine, Mary Mugurusi hakupata kura hata moja  katika nafasi hiyo.

Wakati Diria akishindwa kwa Asmah, Ramadhan Namkoveka ambaye alikuwa katika uongozi wa siku nyingi, mdau huyo wa mchezo wa kuogelea akishindwa kutamba kwa  Inviolata Itatiro alishinda nafasi ya Katibu Mkuu kwa kupata kura 17 huku Namkoveka akipata kura saba tu.

Katika uchaguzi huo Anna Shanalingigwa aliyepata kura 25 kati ya 26 zilizopigwa huku Amina Mfaume akishinda nafasi ya ukurugenzi wa Ufundi kwa kupata kura 19 na kuwashinda Alex Mwaipasi aliyetangaza kujitoa hata hivyo alipigiwa kura (5) na Filex Mosi aliyepata kura moja ambaye naye alitangaza kujitoa pia.

Nafasi ya ukurugenzi wa Elimu na Maendeleo ilichukuliwa na Donald Kweka aliyepata kura 20 kati ya 26. Uongozi huo utakaa madarakani kwa kipindi cha miaka minne.

Viongozi wote waliapishwa kiapo cha utiifu wa uongozi  na Msajili wa Klabu na Vyama Vya Michezo, Ibrahim Mkwawa na kuwataka viongozi hao kuendeleza mchezo  huo.

Mwenyekiti mpya wa TSA, Imani Dominick wadau wa mchezo huo na serikali kwa ujumla kuwa wataleta maendeleo makubwa kwani mpaka kufikia hatua ya kuwania uongozi huo kumetokana na matarajio ya wanachama.

“Lengo ni kuleta maendeleo ya mchezo, nawaomba wanachama kuzingatia Katiba, naomba isomeni na kuifuata,tunaahidi  kuleta maendeleo makubwa,” alisema Dominick.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad