Jeneza lenye mwili wa marehemu Monica Joseph Magufuli likipelekwa Kanisani kwa ajili ya Misa takatifu Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica
Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus
Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga
pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.
Baba Askofu mkuu Mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho
katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani
kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa
heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake
Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani
Geita.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akitoa heshma za Mwisho katika
jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani
Chato mkoani Geita.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkewe Mama Marry Majaliwa wakitoa
heshma zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica
Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akitoa heshma za mwisho
katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha
Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshma
za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika
kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga akitoa heshma za mwisho
katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha
Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsaidia Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani
ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika
kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli
nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo
ndani ya kaburi la Monica Joseph Magufuli wakati wa mazishi
yaliyofanyika katika kijijini cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
shada la maua katika kaburi la Dada yake Monica Magufuli mara baada ya
mazishi.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo
katika kaburi la Monica Magufuli wakati wa Mazishi katika kijiji cha
Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa
Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya
Kikwete akiwa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakati
shuguli za mazishi zikiendelea katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani
Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anazungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazishi ya Dada yake Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment