HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 3 August 2018

NSSF YAPELEKA ELIMU KWA WAKULIMA SIMIYU


Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba akisikiliza maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa NSSF kwenye maonyesho ya Nanenae Simiyu.


NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inashiriki katika maonyesho ya Nanenae yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo, alisema kuwa kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane mwaka 2018 ni 'Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.

Katika maonyesho ya Nanenane Mkoani Simiyu, NSSF inatoa huduma mbalimbali zikiwemo elimu kwa umma juu ya Wakulima Scheme. Lengo la Wakulima Scheme ni kutoa mafao yote yanayotolewa na NSSF kwa wanachama walio katika sekta ya kilimo.

Kwa kujiunga na NSSF wakulima na familia zao wanaweza pata matibabu ya bure, pia NSSF inawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kununulia pembejeo, kusomesha watoto wao na kufanya shughuli zingine za kimaendelo.

Huduma zingine zinazotolewa katika banda la NSSF ni pamoja na elimu ya mafao na umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa watu walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuadikisha wanachama wapya, kutoa taarifa za michango ya wanachama na maelezo juu ya miradi ya nyumba zinazouzwa na Shirika, viwanja na majengo ya kupangisha.

NSSF inawakaribisha wakazi wote wa Simiyu na maeneo ya jirani wafike katika banda la NSSF lililopo pembeni ya mabanda ya Benki ya NMB na NBC ili waweze kupata huduma za NSSF kwa ajili ya kuboresha maisha ya sasa na baadae.
Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

Afisa wa NSSF Khali Abubakar akitoa maelezo kwa mkazi wa Bariadi aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

Afisa wa NSSF Mario Zemba akitoa maelezo kwa mwanachama aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

Afisa wa NSSF Mselem Mwanamsoga akitoa maelezo kwa mwanachama aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad