HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 29, 2018

NDEGE ILIYOKODISHWA ILISHALIPIWA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
RUBANI wa kampuni ya ndege ya Tanzania, (ATCL), Sadiki Jabez, ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, ATCL ililipia garama za matengenezo ya ndege iliyokodisha licha ya kwamba matengenezo hayo yalifanywa na kampuni iliyowakodisha.

 Jabez ambaye pia ni mkurugenzi muendeshaji wa ATCL na  shahidi wa tisa wa upande mashtaka ameeleza hayo leo Agosti 29 wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 71, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustino Rwenzile.

Mattaka anadaiwa kusababisha hasara hiyo kutokana na kusaini mkataba wa kukodi ndege bila kufuata Sheria ya manunuzi ya umma pamoja na ushauri wa kiufundi.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Timon Vitalis, amedai, mwenye jukumu la kutengeneza ndege pale inapokuwa inahitaji marekebisho  hujulikana kutokana na jinsi mkataba ulivyoingiwa lakini hakuwahi kuuuona huo mkataba.

Shahidi Jabez amedai mwaka 2007, ATCL ikiwa chini ya mkurugenzi David Mataka ilikuwa na ndege moja, 737 boing.
 Amedai, baadae ATCL waliazimia kukodisha ndege airbus 320 kutoka kampuni ya Wallis.

Amedai, kutokana na nafasi yake ya mkurugenzi muendeshaji, alikuwa akiingia kwenye mikutano ya bodi ya wakurugenzi kama kisaidia na katika mikutano hiyo hakumbuki kama waliwagi kujadiki juu ya kukodisha ndege na kama ilijadiliwa basi yeye hakuwepo.

Shahidi Jabez ameeleza kuwa Octoba 14.2007 alisafiri baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Mataka aliyewataka kwenda Elsavaldo nchini Uingereza  kwa ajili ya kwenda kuangalia ndege wanayotaka kukodisha.

"Nilienda na Fidelis Tarimo pamoja na John Lyimo kwani unapotaka kukodisha ndege pande mbili ile ya uwezeshaji na wahandisi lazima iwepo kwa kuwa yeye ndio anakagua nyaraka ndani ya ndege inayowezesha ndege kuruka( cooperate) kwani ni rubani ndie anayejua kama ndege inafanya kazi sawa sawa" ameeleza shahidi Jabez.

Ameeleza kuwa, matokeo ya ukaguzi yalionyesha kuwa, ndege ilikuwa inaweza kutumika ila vitu kama viti vilikuwa vinahitaji  marekebisho na vitu vingine vilikuwa vimebomoka.

"Nilimfahamisha mkurugenzi kuwa ndege hiyo ilikuwa inahitaji matengenezo kabla ATCL haijaikodoshwa na mkurugenzi akawaambia kuwa amwambie mkurugenzi wa uhandisi atengeneze mapungufu yote" ameeleza Shahidi.

Ameendelea kueleza kuwa, mtu ambaye huwa na jukumu la kutengeneza ndege anajulikana na jinsi mkataba ulivyoingiwa Ila yeye hakuwahi kuuona huo mkataba na mpaka anaondoka Elsalvado ndege hiyo ilikuwa bado haijafanyiwa marekebisho.

Ameeleza, malipo yote ya kufanyia marekebisho ndege hiyo yamelipwa na ATCL licha ya kwamba matengenezo yalifanywa na kampuni yab Wallis ambayo ndio iliwakodisha ndege hiyo.

Mbali na Mattaka washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Ramadhani Mlinga pamoja na Mkurugenzi wa Sheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka.

Inadaiwa Oktoba 9, 2007 katika ofisi za ATCL Dar es Salaam, Mattaka akiwa Mkurugenzi wa shirika hilo, alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini makubaliano ya kukodi ndege yenye namba A 320-214, kati ya ATCL na kampuni ya Wallis Trading Inc, bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma na taratibu za zabuni.

Aidha anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kusaini makubaliano ya kukodi ndege hiyo bila kufuata ushauri wa kiufundi na kuidhinisha makubaliano hayo, jambo ambalo lilisababisha shirika hilo hasara ya fedha hizo.

Katika mashtaka yanayowakabili, Mlinga na Soka, inadaiwa Machi 19, 2008, katika ofisi za PPRA, Ilala Dar es Salaam, kwa lengo la kufanya udanganyifu, walighushi muhtasari wa kikao cha Machi 19, 2008, kwa lengo la kuonesha siku hiyo, PPRA ilifanya kikao kujadili maombi ya kuruhusu makubaliano ya ATCL kukodi ndege.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad