HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 2, 2018

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA AWAASA WATUMISHI WA TFS KANDA YA KUSINI

Watumishi wa Wakala wa Huduma Tanzania (TFS)  wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi  wakati wanapotekeleza majukumu yao ya uhifadhi.
Rai hiyo imetolewa jana  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipowatembelea jana watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS)  kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya  siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii
Amewataka kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu na yeyote atakayetuhumiwa kupokea rushwa hata kama hajapokea rushwa hiyo kutoka wafugaji kwa makubaliano ya kuingiza mifugo hifadhini kwa makubaliano ya malipo atashughulikiwa ipasavyo.
Aliongeza kuwa endapo watumishi hao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo hakuna kiongozi yeyote watakayesumbuana nao
‘’Tunataka mfanye kazi zenu za uhifadhi  kwa weledi wa hali ya juu na mkifanya vizuri basi nakuwa nimefanya mimi na mkifanya vibaya mnakuwa mnaniangusha mimi hivyo sitokubali’’ alisisitiza Naibu Waziri Hasunga.
Aidha, Amewata wafanye kazi kwa kushirikiana na jamii kwa vile hakuna shughuli yeyote itakayofanikiwa endapo wananchi wataachwa nyuma.
‘’Tunataka jamii ione faida ya moja kwa moja kwa kupata elimu kuhusu uhifadhi pamoja na kushirikishwa kwenye masuala yote ya misitu ili waweze kutoa ushirikiano wakati ukataji miti unapofanyika popote pale’’
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amewataka watumishi hao kuchukua likizo kila mwaka na kuitumia likizo hiyo kwenda sehemu mpya kutalii na kupumzisha akili na kujifunza vitu vipya baadala ya kila likizo kwenda kijiji walikozaliwa kama ilivyozoeleka kwa watumishi wengi.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu, Kanda ya Kusini,  Ebramtino Mgiye alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa  licha ya kuwa na  changamoto ya uhaba wa vitendea kazi lakini kila mtumishi kwa nafasi yake amekuwa akitimiza wajibu wake.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisamiliana na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) wakati alipowatembelea jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga(katikakati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katiak ofisi za Kanda za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwenye ofisi za TFS yao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wa kanda ya Kusini, Ebramtino Mgiye mara baada ya kuwasili jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) wakati alipowatembelea jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga(katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad