HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 13 August 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWAONDOA HOFU WAWEKEZAJI NCHINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamjj.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde amewaondoa hofu wawekezaji na kuwataka kufuata sheria za nchi pindi wanapohitaji kuja kufanya kazi nchini ili kuepuka kusumbuliwa na Serikali .

Mavunde ameyasema hayo kattika Mkutano uliondaliwa na Chama cha Wafanyakazi na Wawekezaji kutoka nchini China kwa ajili ya kuimarisha mahusiano mazuri ya kibiashara.

Akizungumza na wawekezaji hao, Mavunde amesema kuwa amefurahishwa na kukutana baina ya serikali ya Tanzania na Wawekezaji wa China ili kuzungumzia sheria za kazi na vibali vya ukaazi.

Mavunde amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inawahitaji sana wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchini na msimamo wa serikali ni kuleta wawekezaji wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.

Amesema Mavunde," serikali ya Tanzania inawahitaji sana wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi na msimamo wa serikali ni kuoma wawekezaji wanafuata sheria za kazi na ukaazi (uhamiaji) kwa wafanyakazi na wataalamu watakaowaleta na kuona sheria zinafuata sheria za nchi."

Amesema kuwa, anashukuru sana Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kuweza kutafsiri sherianza kazi kutoka lugha ya Kiswahili na kwenda lugha ya Kichina kitu ambacho kitawasaidia sana kutambua kupata elimu na kufahamu sheria za kazi na Ukaazi za hapa nchini.

Akijibu swali la Mwandishi, Mavunde amesema kuwa serikali imekua inatoa vibali ya kazi kwa miaka mitano ila kama Mtaalamu huyo atakuwa bado anahitajika ili watanzania wazidi kupata ujuzi kampuni husika inaweza kukata rufaa na kuelezea sababu na kama zitakuwa na faida kwa Taifa Mtaalamu huyo ataongezewa muda.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa dhumuni la kuwakutanisha wawekezaji na serikali ni kuona biashara zao zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Dkt Mlimuka amesema kuwa hii si mara ya kwanza kwa kufanya mkutano huo na wawekezaji ila kwa sasa wakaamua kuleta na watu wa serikali ambapo amekuja Waziri anayehusika na masuala ya sera, kazi na ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mbali na hilo, ameongezea kuwa uwekezaji mzuri ni ule unaoendana na mazingira mazuri ya kazi pia watanzania waweze kufaidika kwani changamoto zote zinatatulika ikiwemo Ucheweleshaji wa vibali kwa wawekezaji kutokana na kutokuwa na elimu ya sheria za kazi na ukaazi za hapa nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde akizungumza na wawekezaji (hawapo pichani) kuhusiana na taratibu za nchi pindi wanapohitaji kuja kuwekeza na kufanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad