HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 17, 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AHIMIZA USHIRIKIANO BAINA YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU ILI KUONGEZA UFANISI



  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, (katikati), akikokota mpira wakati wa pambano la soka kwenye mazoezi yaliyowashirikisha washiriki wa mafunzo kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa migogoro itokanayo na kazi (CMA) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo Agosti 16, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, amehimiza ushirikiano wa kitaasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Mhe. Mvunde alitoa rai hiyo leo asubuhi Agosti 16, 2018 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuongoza mazoezi yaliyoambatana na michezo mbalimbali ya washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa migogoro itokanayo na kazi (CMA).

“Napongeza ushirikiano huu mliouonyesha kuwezesha mafunzo haya, nawapongeza WCF, na taasisi nyingine mlizoshirikiana nazo katika kutoa mafunzo haya muhimu kwa wafanyakazi wetu, ushirikiano huu ni muhimu kwani wote mnatumikia Ofisi ya Waziri Mkuu.” Alisema Mhe. Mavunde.

Aliipongeza Tume kwa kufanya mabadiliko makubwa katika kupunguza kero baada ya kuja na mkakati wa kupunguza muda katika kufanya usuluhishi. “Hivi sasa mnaanza kuturejeshea heshima ya tume yetu, mimi huwa nashiriki vikao vya wadau wa viwanda na biashara na moja ya changamoto kubwa waliyokuwa wanaisema ni kwenye masuala ya usuluhishi na uamuzi (CMA), kesi zinachukua muda mrefu sana, haziishi kwa wakati na hivyo kuchelewesha ukuaji wa uchumi wa viwanda, lakini haya yalisemwa miaka miwili ile ya mwanzo lakini hivi sasa naona kuna mabadiliko.” Alisema.

Alisema hadi hivi sasa mashauri 9,379 ambayo yalikuja kwa ajili ya usuluhishi, mashauri 7,017 sawa na asilimia 78% yameshughulikiwa na kuamuliwa.

“Haya ni maendeleo makubwa na hii ndiyo iwe spirit ya tume kuona namna bora ya kuweza kuharakisha usuluhishi na uamuzi ili Watanzania wapate haki zao lakini vile vile isaidia kuharakisha huu uchumi wa viwanda ambao kila mmoja tunaamini kwamba ifikapo mwaka 2025 imani ya serikali ni kwamba uchumi wa viwanda utaajiri zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi ya watu milioni 22.3 waliopo Tanzania.” Alisema.

Awali Mhe. Naibu Waziri aliongoza mazoezi ya viungo, mchezo wa soka, kufukuza kuku, kuvuta kamba, kukimbia na magunia.

Mafunzo hayo yameratibiwa na CMA kwa ushirikiano na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).






 Mshindi wa kukimbiza kuku kundi la Wanawake, akiondoka na kuku wake.


 Mbio za kuku.


 Mchezo wa kuvuta Kamba.


 Mchezo wa kuvuta Kamba wanawake



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad