KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo akizungumza kuhusiana na mpango wao wa kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho wakati wa ziara ya viongozi wa bodi Korosho nchini ilipokutana na wakulima wa korosho wa wilaya za Morogoro, Ulanga, Malinyi, Kilosa, Mvomero, Gairo mkoani Morogoro na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora.
Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba kulia akimsikiliza mmoja wa wakulima wa zao la Korosho mkoani Morogoro mara baada ya kuwatembelea wakulima na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora.
KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo kushoto akiagana na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana mara baada ya kufanya mazungumzo naye.
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana kulia akisalimiana na wakulima wa zao la Korosho mkoani Morogoro mara baada ya kuwatembelea na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora
NA MWANDISHI WETU, MOROGORO.
KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji
ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo amesema mkoa huo
umejipanga kufanya uhamasishaji na ufuatiliaji wa zao la Korosho ili
kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kuliko iliyokuwa miaka iliyopita
Mkondo aliyasema hayo wakati wa bodi Korosho nchini
ilipokutana na wakulima wa korosho wa wilaya za Morogoro, Ulanga,
Malinyi, Kilosa, Mvomero, Gairo mkoani Morogoro na kutoa elimu namna
bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo
bora
Ambapo alisema uhamasishaji huo utashirikishi wakuu
wa wilaya na viongozi wengine wa ngazi za chini kwa lengo la
kuhakakikisha kilimo hicho kinalimwa kwa tija kubwa ili kuweza
kuwasaidia kuwainua wakulima kiuchumi..
Alisema licha ya
kwamba wana wataalamu wana upungufu mkubwa wa wataalamu wa kilimo
kwenye maeneo ya vijijini wakati wanawasubiri wanachofanya wamewagawa
wa maeneo ya kata na Vijiji ili kuwasaidia kuongeza nguvu kutoa
ushauri wa ugani kwa wakulima “Anasema
Aidha alisema hivi
sasa wanawahimiza wataalamu waliopo ngazi za kata wafike kwenye maeneo
ya vijiji kutoa ushauri hasa mashamba darasa hilo litasaidia kutoa
elimu inayohusika kwenye mazao mbalimbali ikiwemo zao la korosho.
Mkondo alisema wanalifanya hilo kwa kushirikiana na bodi ya
Korosho na maafisa ugani ambao hawajapata elimu juu ya uzalishaji huo
wanaitwa na kupewa elimu juu ya zao husika ili waweze kujua namna ya
kuwaelimisha wakulima.
Akizungumzia suala la malipo
yanayofanywa na bodi ya korosho alisema licha ya kuwepo kwa changamoto
lakini wamehaidi kuanza kuyashughulikia kwa kuanza kufanya uhakiki ili
waweze kujua vikundi vipi vimezalisha na baadae waweze kulipwa malipo
halali.
“Lakini kama uhakiki umekwisha kufanyika bodi ya
korosho na umekamilika malipo yafanyike kwa wakati ili vikundi viweze
kulipwa kwa haraka huku akisisitiza kwamba pembejeo zinasambazwa na
serikali kupitia bodi ya Korosho hivyo wakulima wafuatwe taratibu
zilizopo waweze kupata pembejeo hizo”Anasema
Aliongeza
kuwa mwaka jana mkoa huo uliweza kustawisha vitalu 36 vya korosho
ambavyo walipata miche 702,000 ilioteshwa na vikundi mbalimbali
vilivyopata msaada kutoka bodi ya Korosho lakini waliweza kupata mbegu
za kupanda kilo 4154.
Alisema baada ya kupata mbegu hizo
waliweza kusambazwa na kupandwa na wakulima kutokana na uhamasishaji
katika mkoa kuwa mkubwa zaidi kama kutokana na wananchi kuitikia
mwitikio mzuri wa kuweza kulima zao hilo.
No comments:
Post a Comment