HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 14, 2018

MHANDISI NDIKILO AWAAHIDI UMEME WA REA AWAMU YA TATU KUWAFIKIA WANANCHI WOTE WA PWANI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis  Evarist Ndikilo amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Matimbwa kata ya Yombo kuwa awamu ya tatu ya Mradi wa  Umeme wa vijijini REA utawafikia wale wote walikosa.

Hayo aliyasema mbele ya wananchi wa Kijiji hicho akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Zainab Kawawa na Diwani wa Kata hiyo Mohamed Abdallah Usangi

Amesema kuwa, katika awamu ya kwanza na ya pili wananchi baadhi waliweza kupata umeme huo wa bei rahisi na wengine walikosa ila katika awami hii ya tatu watapita kwa ajili ya kuangalia wapi panahitajika kuwekwa nguzo za umeme.

" Awamu ya kwanza na ya pili ya umeme wa REA ilipita na ni kweli kuna baadhi ya wananchi au maeneo bado hayajafikiwa na mradi huu ila katika awamu tatu watapita kuona mahali ambapo nguzo za umeme hakuna na kuanza mchakato wa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme," amesema Mhandisi Ndikilo.

Mhandisi Ndikilo amesema kuwa, mbali na kuwaahidi wananchi hao bado atawasiliana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na kuweza kufika nae kwa wananchi hao ili awahakikishie umeme utafika kwao hapo lini.

" ni kweli umeme utakuja hapa ila uzuri ni kuwa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ni mtoto wenu, mtoto wa Pwani hapa hapa atakuja na kuwahakikishia watu wa kata ya Yombo kuwa umeme utafika mpaka hapa na serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuona wananchi wanapata huduma zinazostahiki," amesema Mhandisi Ndikilo.

Hayo aliyajibu baada ya hoja ya Diwani wa Kata ya Yombo Mohamed  Usangi kuulizia mradi wa umeme wa vijijini REA ambapo kuna baadhi ya wananchi wa kata yake bado  hawajafaidika na mpaka sasa huku wakikosa huduma ya umeme.

Mbali na hilo, Mhandisi Ndikilo alijibu swali la Diwani Usangi kuhusiana na madereva wa bodaboda kukamatwa mara kwa mara na faini zao kulipishwa kubwa sana tofauti na magari ya abiria yakikamatwa.

Amesema, suala hilo ni la RPC wa mkoa lakini kwa namna ya kawaida dereva wa bodaboda anatakiwa afuate sheria ikiwemo kuvaa helment (kofia ngumu) avar viatu vilivyofunika pamoja na kuwa na leseni lakini madereva wengi wamekuwa hawajakamilisha vitu hivi, ila amesikia changamoto hiyo inayowakumba vijana na amewaahidi wananchi wa Kata ya Yombo kushirikiana nao na  kuweza kutatua tatizo hilo ikiwemo kutoa elimu kwa vijana wanaoendesha pikipiki hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis  Evarist Ndikilo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Matimbwa kata ya Yombo Wilayani Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad