HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 17, 2018

MBUNGE CCM AIBUA UFISADI WA MILION 176 KWENYE ZIARA YA WAZIRI MKUU IGUNGA

Na Francis Daud, Manonga-Tabora
MBUNGE wa Jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameibua ubadhirifu mkubwa wa fedha uliofanyika ndani ya jimbo lake mbele ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa ziarani Mkoani Tabora.

 Akihutubia mbele ya mamia ya wananchi wa Manonga waliokuwa wakimshangilia muda wote Gulamali amemweleza Waziri Mkuu kuwa  kuna upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 140 mali ya kijiji cha Bulagamilwa.

Gulamali amesema kuwa fedha hizo ambazo zilikusanywa kama mrahaba wa machimbo ya madini yaliyopo katika kijiji hicho na hata hivyo baada ya kelele za wananchi, mtendaji wa kijiji alihamishwa toka kijijini hapo baada ya wananchi kukosa imani na utendaji wake.

Aidha Mbunge huyo alifumua mradi mwingine wa ujenzi wa mashine za kukoboa mpunga katika kata ya Choma Chonkola na  Alimweleza Waziri mkuu kwamba, zaidi ya milioni 35 hazijulikani mpaka leo zilipokwenda na hakuna mashine iliyofungwa.

Akilitolea maelezo suala hilo, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora  aliposimamishwa na waziri mkuu kujibu tuhuma hizo alisema ni kweli wana faili hilo na bado wanaendelea kukusanya taarifa muhimu kabla ya kufungua mashtaka kwa wahusika.

 Maelezo hayo hayakuridhisha umma wa wana Manonga na Waziri mkuu akatoa maagizo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa, Ntemi James kwa kuwa ndiye mtuhumiwa wa kwanza katika sekeseke hilo la upotevu wa  shilingi Milion 141 za kijiji hicho.

Aidha, Waziri mkuu amemwagiza OCD wa wilaya ya Igunga kuwasweka ndani viongozi na kamati iliyohusika na upotevu wa milioni 35 zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Igunga kwa ajili ya uwekaji wa mashine za kisasa za kukuboa mpunga katika kata ya Choma Chonkola.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akizungumza na wananchi mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili jimboni hapo katika ziara yake Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiwa na viongozi mbalimbali wakingozwa na Mbunge wa Manonga Seif Gulamali, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad