Marafiki wa Wafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Karim Mchaka, Athuman
Said, Nathan Mpangala na Ndalo Kalua wakijadiliana jambo wakati wa zoezi
la usafi wa jumla katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu,
Mtwara hivi karibuni.
Wanawafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Athuman Said, ndilo Kalua na
Winny Majuva wakihamisha vitanda kutoka katoka wodi ya watoto ili
kupisha uchoraji hivi karibuni.
Marafiki wa Wafanye Watabasamu, kutoka kushoto, George Nyandiche, Nathan
Mpangala na Winny Majuva wakifanya yao kwenye wodi ya watoto ya
Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Kutoka kushoto, George Nyandiche, Neema Loth, Asteria Malinzi na Masoud
Kibwana wakiendelea na uchoraji katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya
Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Wazazi wakiwa na watoto wao katika wodi ya watoto ya Hospitali ya
Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara mara baada ya Marafiki wa Wafanye
Watabasamu kumaliza kupamba wodi hiyo kwa michoro hivi karibuni.
Wazazi pamoja na watoto wao wakifurahia muonekano mpya wa wodi ya watoto
ya Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hamis Dambaya (mwenye shati
mikono mirefu) akiwa katika picha ya pamoja na Wanawafanye Watabasamu na
baadhi ya viongozi mara baada ya kukamilika kwa uchoraji katika wodi ya
watoto Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara. (Picha zote na
NMF)
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Nathan Mpangala Foundation (NMF), kupitia programu yake ya Wafanye Watabasamu, hivi karibuni ilishirikisha marafiki wa programu hiyo kubadilisha mwonekano wa wodi ya watoto na chumba cha daktari wa watoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara toka kuta nyeupe na kuwa zenye michoro mbalimbali.
Mwenyekitio wa taasisi hiyo, Nathan Mpangala alisema lengo la kazi hiyo ya siku tano mbali na kuichukulia kama ibada pia ililenga kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuipa wodi ya watoto ya hospitali hiyo mazingira rafiki kupitia sanaa ya uchoraji, kurudisha kidogo walichonacho kwa jamii na kuhamasisha umuhimu wa matumizi ya sanaa ya uchoraji kwenye maeneo yanayotoa huduma ya afya.
“Zahanati, vituo vha afya na mahospitali uhudumia wagonjwa. Mara nyingi huwa na maumivu, uchovu, upweke na msongo wa mawazo. Sehemu hizo zinapokosa michoro ukutani ambayo ingeweza kuwasahaulisha maumivu, hali huwa ngumu zaidi kwao. Sanaa si kwa ajili ya wagojwa tu, ni muhimu pia madaktari, wauguzi na wote wanaohusika na huduma ya afya. Kama maofisini, kumbini, sebuleni, hotelini tunaning’iniza sanaa iweje zinakosekana sehemu nyeti kama mahospitalini?” alihoji Mpangala.
Mpangala anaishukuru Toyota Tz, Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na marafiki mbalimbali wa NMF kwa kuwezesha tukio hilo na kwamba ametoa wito kwa wadau na wananchi kujitokeza kushirikiana na taasisi yake. “NMF ina mtandao mkubwa wa wachora nchini na wako tayari kujitolea kwa kushirikiana na wananchi au vikundi vilivyo tayari kujitolea.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hamis Dambaya akizungumza wakati wa zoezi hilo alisema, michoro kwenye wodi za watoto ni muhimu kwani huwaondolea uwoga hivyo kuna umuhimu wakazingatia hilo wakati wa kutengeneza na bajeti zetu.
Aidha, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Furaha Mwakafwila, ameishukuru NMF kwa kuchagua hospitali yake. “Hospitali ziko nyingi nchini, lakini mmeamua kuja kwetu. Tumefurahishwa na moyo wenu wa kujitolea. Karibuni tena siku nyingine,” alisema.
No comments:
Post a Comment