Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu
Mhe. Jaji Sylvain Ore muda mfupi kabla ya kuapishwa kwa Majaji wapya
watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa hafla ya kuapishwa kwa majaji wapya watatu
wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mjini Arusha.
Majaji watatu wapya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu
wakiwa wameketi pamoja muda mfupi kabla ya kuapishwa, kutoka kushoto ni
Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam
(Nigeria) na Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania). (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu na Watu Mhe. Jaji Sylvain Ore mara baada ya kuapishwa kwa
Majaji wapya watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha mpya na Majaji wateule wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambao wameapishwa leo mjini Arusha kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania) na kulia ni Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria) . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment