HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 15, 2018

KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA, MAZINGIRA KUFANYIA KAZI MPANGO WA ETS.

MPANGO wa uwekaji muhuri wa Kiectroniki ya kodi (Electronic tax stamp(ETS) kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa watengenezaji wa pombe kali kwani waingizaji wa pombe kali wa kinyemela hawatanufaika katika soko la pombe kali hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa TBL kitengo cha utengenezaji wa Konyagi, Davis Deogratius wakati akitoa ripoti ya kiwanda cha kutengeneza bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) jijini Dar es Salaam leo wakati wajume wa kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho jijini Dar es Salaam.

"ETS itasaidia sana kwa watengenezaji wa pombe kali hapa nchini na ukusanyaji wa mapato ya serikali utaongezeka kwani kunapombe kazi zinauzwa kinyemela hapa nchini."

Nae Naibu waziri wa wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji, Mhandisi Stela manyanya w
ataishauri serikali ili mpango huo wa ETS ufwate ili kudhibiti uingizwaji wa pombe kali kinyemela na kuuza bia serikali kupata kodi.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa kamati ya Viwanda,biashara na mazingira  ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Innocent Bashungwa amesema kuwa viwanda vyote vya kutengeneza Mvinyo pamoja na Pombe kali lazima wafuate mpango huo kabambe wa ETS ili serikali kupata mapato stahiki.

Pia baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza utendaji kazi wa kiwanda cha TBL kwani mitambo mingi inatumia technolojia ya hali ya juu kwaajili ya kukidhi utendaji wao wa kazi.


 Meneja Mkuu wa TBL kitengo cha utengenezaji wa Konyagi, Davis Deogratius akizungumza   wakati akitoa taarifa ya kiwanda cha kutengeneza bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) leo mara baada ya kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutembelea katika kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Baandhi ya wafanyakazi wa TBL pamoja na wabengu walipotembelea kiwanda cha TBL leo wakmsikiliza Meneja Mkuu wa TBL kitengo cha utengenezaji wa Konyagi, Davis.
 Makamu mwenyekiti wa kamati ya Viwanda,biashara na mazingira  ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Innocent Bashungwa akizungumza kwaajili ya kufungua kikao kilichohusihsa wabunge pamoja na wafanyakazi wa TBL jijini Dar es Salaam leo.
Naibu waziri wa wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji, Mhandisi Stela manyanya  akizungumza mara baada ya kusikiliza ufafanuzi kutoka kwa Innocent Bashungwa akitoa taarifa ya kiwanda cha kutengeneza bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) leo jijini Dar es Salaam wakati kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kujionea jinsi wanavyotenda kazi pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.



 Wajumbe na kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira na wabunge wa bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania wakipata malezo wakati wakitembelea Kiwanda cha TBL jijini Dar es Salaam leo.


 
 Wajumbe na kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira na wabunge wa bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania wakitembelea kiwanda cha TBL jijini Dar es Salaam leo.









 Mtambo unaosafirisha Bia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

 Mtambo

 Mtambo unaojaza bia kwenye chupa.
 Mtambo unao panga chupa kwenye Makreti ya bia.

 Mitambo mbalimbali ya kutengeneza bia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad