HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 13 August 2018

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA YATEMBELEA KIWANDA CHA ALAF JIJINI DAR ES SALAAM LEO

KAMATI viwanda ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetembelea kiwanda cha kutengeneza mabati cha ALAF jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo iliyohusisha wabunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo ya bunge ilikuwa na leongo la kuangalia utendaji kazi wa kiwanda cha Kutengeneza mabati cha ALAF pamoja na Kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakumba katika uendeshaji wa viwanda vya hapa nchinni.

Mwenyekiti wa Kamati ya viwanda ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Suleiman Ahmed Sadiq akizungumza na wabunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo amesema kuwa serikali inapaswa kuhakikisha kuwa umeme unakuwa wa uhakika ili kukuza viwanda hapa nchini.

Pia amesema kuwa serikali ikae na wenye viwanda vya ndani ili kuhakiki gharama za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani ili kuzuia bidhaa za enje ya nchi kuuzwa kwa gharama ya chini kuliko ya viwanda vya ndani ya nchi.

"Serikali ikae na wenye viwanda ili kuhakiki bei za uzalishaji wa bidhaa kwaajili ya kuweka bei nzuri kwa watumiaji wa bidhaa hizo za viwandani".

"Pia sisi kama wabunge tutakaa na serikali kwajiili ya kuishauri na kuieleza ni sehemu gani kunamianya ya uongezaji wa bei za bidhaa za viwandani".
Kamati hiyo ya viwanda itatembelea viwanda tisa vilivyopo hapa nchini.

Kwa upande wao kiwanda cha ALAF wameiomba serikali na shirika la Viwanda kuangalia bidhaa zenye viwango zinazoingizwa hapa nchini ili kuwa na soko linalolingana pia wameiomba serikali kuwa na umeme wa uhakika ili kukuza viwanda vya nyumbani pamoja na kukuza uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Mwenyekiti wa Kamati ya viwanda ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Suleiman Ahmed Sadiq akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha ALAF Tanzania wakati kamati hiyo ya bunge ilipotembelea katika kiwanda hicho kwaajili ya kuangalia chamangamoto wanazokumbana nazo pamoja na kuangalia vikwazo mbalimbali ambavyo vinasababisa viwanda vya ndani visukue zaidi.
Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biasharana viwanda prof. Joseph Buchweishaija akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha ALAF mara baada ya kamati ya viwanda ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam leo.


 Baadhi ya wabunge na wajumbe wa kamati ya Viwanda ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiuliza maswali kwa Mkurugenzi Mkuu wa ALAF Dipt Mohanth hayupo  pichani wakati wa kamati hiyo ya Bunge kufika katika kiwanda cha kinachozalisha mabati cha ALAF leo.
 Baadhi ya wajumbe na wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ALAF, Dipt Mohanty jijini Dar es Salaam leo walipotembelea kiwanda cha ALAF.
.
 Baadhi ya wabunge na wajumbe wa kamati ya Viwanda wakielekea kukagua na kuangalia jinsi kiwanda cha kutengeneza mabati cha ALAF kinavyofanya kazi. ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa kamati ya wizara ya viwanda na biashara, prof. Joseph Buchweishaija akipata(kulia) akipata aelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa Kiwanda cha ALAF mara baada ya kamati ya viwanda ya bunge kutembelea katika kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanakamati ya viwanda wakipata maelekezo walipo tembelea kiwanda cha kutengeneza Mabati cha ALAF jijini Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha ALAF wakiendelea na kazi.


  Wabunge na wajumbe wa kamati ya viwanda wakiwa ndani ya kiwanda kujionea utendaji kazi wa kiwanda cha ALAF hapa nchini.
 Baadhi ya Bidhaa za kiwanda cha ALAF. 
 Baadhi ya Mitambo ya kutengeneza bomba za mstatili kwaajili ya kutengenezea mageti.
Baadhi ya mitambo ya kiwanda cha ALAF.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza Mabati cha ALAF, wakiongozwa na Shomari Katundu(katikati). 

Baadhi ya wabunge, wajumbe na wafanyakazi wa Kiwanda cha ALAF wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kamati ya Bunge ya viwanda ilipotembelea kiwanda cha ALAF jijininDar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad