HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 16, 2018

KAIMU RAIS TCCIA AISHAURI SERIKALI KUTAMBUA MCHANGO KATIKA SEKTA BINAFSI KUKUZA UCHUMI


Na Mwandishi wetu
KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu ameiyomba Serikali kutambua mchango  katika sekta binafsi (TPSF) katika kukuza uchumi wa nchi hususani katika suala la Biashara na masoko.

Aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi mtendaji wa TPSF, Dk. Geofrey Simbeye kuusu maadhimisho ya kutimiza miaka 30 ya kuazishwa kwa taasi ya TCCIA ambapo TPSF nao wataadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa.

Mshiu alisema serikali ya amwamu ya tano imekuwa ikitoa fursa za uwekezaji katika kampuni mbalimbali za nje ya nchi katika ujezi wa miundo mbinu hivyo kama wanaomba watambue taasisi hizo katika kukujenga uchumi ndani ya nchi.

“Watu wote tupo katika kuakikisha uchumi wa nchi yetu ianakuwa hivyo kama tukiwa na ushirikiano katika sekta binafsi na serikali lazima tutapata maendeleo,” alisema.

Aidha Mshiu alisema wanatarajia kufanya sherehe ya pamoja tangu kuazishwa kwa TCCIA miaka 30 kwa kuungana na TPSF  ambao nao wanatimiza miaka 20, lengo likiwa ni kuangalia namnagani sekta binafsi zimeweza kusaidia maendeleo ndani ya nchi na kwa wafanya biashara.

Alifafanua kuwa TCCIA ndio waazilishi wa TPSF hivyo katika sherehe hizo zinazo tarajia kufanyika Novemba mwaka huu watalenga namnagani wadau na wafanyabiashara wamefanikiwa .

Nae Mkurugenzi  wa TPSF, Dk.Simbeye alisema ushirikiano wa taasisi hizo umelenga kuimarisha ukuwaji wa maen deleo kwa wafanyabiashara .
Alisema kupitia kauli mbalimbali za serikali ya Rais Magufuli alizokwisha kutoa kwa wafanya biashara kuwekeza katika awamu hii ni wazikuwa ndio fursa ya peke ndani  kwa wana chama wa taasisi hizo kuakikisha  wanafungua viwanda  .
Hata hivyo Dk Simbeye amewataka wafanya biashara kujitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika hawamu ya tano ili kukuza uchumi maana ndiyo awamu pekee iliyowapa wawekezaji kipaumbele
 Mkurugenzi wa TPSF Godfrey Siambeye kushoto akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa Biashara na kukuza uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa, kulioa ni KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu
Mkurugenzi wa TPSF Godfrey Siambeye kushoto, kulia ni KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu wakipongeza mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa Biashara na kukuza uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad