HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 13, 2018

DKT. BASHIRU ATOA SHUKRANI BAADA YA UCHAGUZI, AMPOKEA KUCHAMKA AKITOKEA CUF



Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa shukrani wa wananchi wanaoendelea kuunga mkono katika shughuli zao za kuimarisha chama.

Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi ndogo za chama Lumumba jijini Dar es salaam Bashiru ameeleza kuwa chaguzi ndogo chama chao kimekuwa na mvuto tena na hii ni baada ya chama cha mapinduzi kujizolea ushindi katika jimbo la Buyungu na kata zote 77 zilizokuwa zinafanya uchaguzi wa marudio ambapo kata 41 walipita bila kupingwa na kata 36 walifanya uchaguzi na kushinda kwa kishindo na hata katika kata ambazo hazijawahi kutwaliwa na chama cha mapinduzi tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka huu zimechukuliwa na CCM.

Aidha ameeleza kuwa wanafanya vizuri kwa kuwa wafanyayo yanawapa tumaini walio wengi hasa wanyonge na shabaha zao zipo katika kupambana na umaskini, kuongeza nafasi za ajira hasa katika sekta za kilimo na ufugaji, na kupambana na rushwa na ufisadi.

Pia amehimiza mshikamano ndani ya Chama kwani hadi sasa chama kimerejea katika misingi ya waasisi wake kwa kutekeleza misingi ya utu, usawa, na usawa. Na amewahaidi watanzania kufanya kazi na kutobweteka usiku na mchana.

Wakati huo huo Dkt. Bashiru amempokea aliyekuwa Mbunge wa Liwale kupitia tiketi ya CUF Zuberi Mohamed kuchamka kuwa mwanachama mpya wa CCM.

Zuberi ameeleza kuwa amehamia CCM kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais ambapo ndani ya miaka 2 katika jimbo lake la Liwale wamepata huduma za msingi zikiwemo afya na utatuzi wa migogoro na akaona hana budi kufuata kasi hiyo na amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi wampokee wafanye kazi.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza mda mfupi kabla ya aliyekuwa Mbunge wa CUF katika jimbo la Liwale mkoani Lindi Zuberi Kuchauka (kulia), kutangaza kukihama Chama cha Civic United (CUF), na kujiunga na CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad