HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 30 August 2018

DC SOPHIA MFAUME ATEMBELEA SEKONDARI YA NASULI, AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIKE, AELEZA MIKAKATI

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume  akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma leo Agosti 30,2018.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvumawakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume katika wilaya hiyo leo Agosti 30,2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume akimsikiliza mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli leo. 
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume akikabidhiwa taarifa ya shule ya sekondari Nasuli na mkuu wa shule hiyo. 

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume ametembelea Sekondari ya Nasuli yenye kidato cha kwanza hadi cha sita iliyokuwa kwanza kimkoa katika matokeo ya Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) mwaka jana.

Akiwa shuleni ametumia nafasi hiyo pia kueleza kuwa malengo yao ni kuhakikisha shule hiyo inashika nafasi ya kwanza kitaifa huku akitoa ushauri kwa wanafunzi wahakikishe wanasoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana uhusiano na masomo.

Akizungumza leo na Michuzi Blog, DC Mfaume amesema ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanafunzi kwamba kitu chochote kikikaa eneo lisilo sahihi kinakua uchafu.

Amewapa mfano kwamba “Karatasi safi nyeupe nikiichukua na kuitupa pale 'smart area' ya shule basi itageuka na kuwa uchafu.... hivyo hata kuchanganya masomo na mambo yasiyohusu inakua ni uchafu.”

Mfaume amewasisitiza wanafunzi wa kike kuzingatia kanuni ya magauni manne ili wafikie ndoto zao.

Amefafanua gauni la kwanza ni sare za shule, gauni la pili ni joho kwa wanaohitimu Chuo Kikuu, gauni la tatu ni la harusi na gauni la nne ni nguo ya kwenda kujifungua.

Hivyo kwa sasa watambue gauni lao ni sare za shule za sekondari na wasikubali kuchanganya na magauni mengine kwani itakuwa ni uchafu na itawaharibia kufikia malengo yao.

Pia amewakumbusha kuzingatia nidhamu, bidii na kutokata tamaa huku akifafanua ni viungo muhimu katika kuhakikisha wanafaulu katika masomo yao na maisha kwa ujumla.

Amewaambia yeye akiwa shuleni alihakikisha anasimama katika kutimiza ndoto zake , hivyo aliweka kando kila aina ya uchafu na hatimaye alifanya vema kwenye masomo kwa kupata ufaulu mzuri.

Pia amesema amepata nafasi ya kuzungumza na walimu kwa kuweka mikakati itakayofanikisha shule hiyo kufanya vema kwenye mtihani wa Taifa kwa kushika nafasi ya kwanza.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad