HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 15 August 2018

CRDB BANK YAWAPIGA MSASA WA MWISHO WAJASIRIAMALI WANAWAKE WAFUGA KUKU

Meneja Mwandamizi Dawati la Akinamama wa CRDB Bank, Rehema Shambwe (kulia), akielezea sera za benki hiyo, kwa Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakati wa siku ya ufungaji wa semina yao, ya siku mbili inayokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Flex Gardern. Semina hiyo, imefungwa na Mbunge wa jimbo hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega. CRDB Bank imedhamini semina hiyo.
Baadhi ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakimsikiliza Meneja Mwandamizi Dawati la Akinamama, Rehema Shambwe, alipokuwa akizungumza nao kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo, kwa wateja wake.


Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam, Midlaster Nsanzugwanko, akizungumza na Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga katika siku ya mwisho ya semina hiyo, kuhusu kutoa mikopo mbalimbali ya kuwawezesha kufikia malengo yao, ya kuwa wafugaji wa kutegemewa na taifa.

Mwakilishi wa Taasisi za US CEVA Animal Health na US Grains Ancil Tanzania, Dk. Peter Makang'a, akitoa elimu kuhusu ufugaji bora na vyakula gani na vyenye virutubisho gani vinafaa kwa ufugaji kuku. Pia aina za dawa zinazofaa kutumiwa kwa mifugo katika kuwafanya kutopata maradhi ya kuambukiza.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya uuzaji wa vyakula na dawa za mifugo ya Farmers Centre, Muhsin Awadhi, akitoa maelezo ya dawa mbalimbali za mifugo kwa wanasemina, Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, waliofika kwenye banda lao katika siku ya ufungaji wa semina yao hiyo. Kampuni hiyo, ni moja wa wadhamini wa semina hiyo.
Baadhi ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakiwa kwenye banda la CRDB Bank kupata huduma mbalimbali, zikiwemo za kujiunga na benki hiyo.
Wanasemina Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakicheza kwa furaha wakati wakitoka kumpokea mgeni rasmi katika ufunguji wa semina yao, Mbunge wa jimbo hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega.
Mgeni rasmi katika ufungaji wa semina hiyo, Mbunge wa Mkuranga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akipongezwa kwa kupeana mikono na wanasemina hao, Wajasiriamali wanawake wafuga kuku.
Mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akizungumza na Wanasemina Wajasiriamali wanawake wafuga kuku, wakati akiifunga semina yao hiyo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega, wa tatu ni Makamu Mwenyekiti wa Jikwaa, Christina Mrema na kushoto ni Mhazini wa Jukwaa, Shufaa Msangi.


Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wao, Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, jijini Dar es Salaam, Midlaster Nsanzugwanko.

Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega (katikati), akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abeid (kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wake Afisa Maendeleo ya Jamii, Mkuranga, Safina Msemo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wao, Mwakilishi wa Benki ya NMB, Mkuranga, Halima Nkya.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akiwaeleza jambo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega (katikati) na Makamu wake, Christina Mrema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad