Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda, amewasili nchini kwa ajili ya kufanya maonyesho tofauti katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.
Werrason aliyewasili majira ya saa sita mchana akipokelewa na mamia ya watu pamoja na msanii wa muziki wa dansi nchini King Dodoo na mratibu wa ziara hiyo Lengos VIP.
Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JKNIA, Werrason amesema kuwa amekuja kukata kiu ya wapenzi wa muziki wa dansi nchini ambao walimkosa katika shoo iliyopita
Amesema kuwa shoo yake ya mwisho alishindwa kuja ila kwa sasa amekuja kuleta burudani iliyokosekana baada ya kushindwa kufika.
"Nimekuja kukata burudani ya wapenzi wa soka baada ya kukosekana kwa shoo ya mwisho ila sasa hivi nipo na nimeshafika hapa wajiandae kwa burudani,"amede
Naye Mratibu wa ziara ya mwanamuziki huyo, King Dodoo Labuche alisema kuwa mwanamuziki huyo amewasili tayari na ataondoka kesho mapema kuelekea Mkoani Arusha kwa ajili ya shoo ya Kwanza na kisha siku ya Jumamosi atakuwa mkoani Mwanza na ya mwisho atamalizia hapa Dar es Salaam.

"Werrason atafanya Shoo ya kwanza mkoani Arusha siku ya Ijumaa ya Julai 6 na siku ya pili ya Julai 7, atakuwa mkoani Mwanza huku onyesho la mwisho litafanyika Mkoani Dar es Salaam'"amesema King Dodoo Labuche
Alisema mkoani Arusha Mwamuziki huyo atafanya onyesho kwenye ukumbi wa Mjengoni Club, wakati Mwanza atafanya mambo yake kwenye ukumbi wa Rock City na Mkoa wa Dar es Salaam Life Park uliopo Mwenge (zamani Word Cinema)..
Werrason aliyeanzia katika bendi ya Wenge BCBG, miongoni mwa wanamuziki wa Congo wanaopata nafasi za kupata mwaliko wa kuja kutoa burudani hapa nchini, huku mratibu wa maonyesho hayo akiwataka mashabiki wajitokeze kupata burudani nzuri kutoka kwa nguli huyo.
Mratibu wa Ziara ya Mwanamuziki Werrason King Dodoo Labuche akizungumza na waandishi wa habari baada ya msanii huyo kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa ajili ya maonyesho yake sehemu tofauti nchini.
Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa ajili ya maonyesho yake sehemu tofauti nchini.

No comments:
Post a Comment