HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 8, 2018

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
SERIKALI imewaagiza wataalamu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) kutoa majibu kuhusu upotevu wa maji unaosababisha hasara kubwa kwa Serikali.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Process Makame Mbarawa ameagiza hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya maji iliyopo chini ya Dawasa ya Ruvu Juu na Ruvu chini.

Profesa Mbarawa ameeleza  licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya kumaliza tatizo la maji, Dar es Salaam na Pwani, asilimia 44 ya maji kati ya lita milioni 504 zinazozalishwa kila siku katika vyanzo mbali mbali hupotea kabla ya kufika kwa mtumiaji wa mwisho.

 Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, takribani bilioni nne hupotea kila mwezi kutokana na upotevu wa maji hayo, upotevu ambao ni mkubwa wakati wananchi wakiwa hawana maji. 

"Serikali inapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa maji njiani kabla ua kufika kwa mtumiaji wa mwisho, ni wakati umefika sasa kwa wataalumu wetu kumaliza tatizo na kutoa majibu yanayoeleweka, lazima Tuingie kwa undani tuangalie maji haya yanapotelea wapi" amesema Profesa Mbarawa

Amesema kama wataalamu wanatakiwa kuja na majibu ya uhakika na haraka na yaliyochunguzwa vizuri.
Pia asema pamoja na kuzalisha kiwango kikubwa cha maji katika miradi yote ya Dawasa ni lita milioni 504 kwa siku lakini mahitaji ni lita milion 544 hivyo kuna upungufu ni lita milioni 44 0 kwa siku. 

Aidha amewakikishia wakazi wa maeneo ya Kibamba na Kiluvya wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam ambao wamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa kuwa kuanzia Agosti mwaka huu watapata maji ya uhakika masaa 24, siku saba za wiki, kwa mwaka mzima.

Kwa mujibu wa Dawasco, awali tatizo la upotevu maji lilikuwa asilimia 57  na limeshuka hadi asilimia 44 na  malengo yao ni kupunguza tatizo hadi asilimia 30 ifikapo mwaka  2030.

Wakati huo huo, Profesa Mbarawa  amempongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kumteua Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Dawasa.

"Mwamunyange ni mtu imara, ninaamini ataleta mapinduzi katika taasisi ya Dawasa na kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam  na mikoa ya Pwani wanapata maji safi na salama wakati wote." amesema Profesa Mbarawa.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akikagua mtambo wa Ruvu Chini, wakati wa ziara yake ya kikazi, Ruvu, mkoani Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu mtambo wa mpya wa Ruvu Juu wa kudhalisha maji, mkoani Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukagua kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
Mkazi wa Kiluvya, wilayani Ubungo, akitoa malalamiko yake kuhusu mfumo wa kulipia maji unaotumiwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), unavyowasumbua wananchi kupata huduma ya majisafi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad